Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi akiwasilisha Mada kuhusu Mawasiliano ya Kimkakati ya Serikali katika Zama Mpya za Utekelezaji Mei 27, 2021 katika Kikao Kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini Jijini Mbeya.
************************
Na Shamimu Nyaki, Mbeya
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan amewataka Maafisa Habari katika Wizara, Mikoa, Halmashauri,Taasisi, Mamlaka na Wakala za Serikali kuzisemea taasisi zao ili zitambulike kwa huduma wanazotoa kwa wananchi.
Dkt. Abbasi amesema hayo alipokuwa akiwasilisha mada inayohusu Mawasiliano ya Kimkakati ya Serikali katika Zama Mpya za Utekelezaji Mei 27, 2021 Jijini Mbeya ambayo lengo lake ni kuwajengea uwezo maafisa hao waweze kusemea taasisi zao kimkakati.
“Afisa Habari ni lazima uelewe taasisi yako, maelekezo mapya yanayoingia katika taasisi na namna ya kuyafanyia kazi na mtambue jukumu lenu ni kutoa taarifa kwa kuzingatia Sheria za ndani na nje ya nchi ikiwemo Mkakati wa Kimataifa wa Haki za Kisiasa na Kiraia, hivyo ni lazima muwajibikeamesema Dkt. Abbasi.
Dkt. Abbasi ameongeza kuwa Serikali lazima iaminike na kukubalika kwa wananchi wake, hivyo utoaji wa taarifa utasaidia Serikali kuaminiwa na wananchi,huku akisisitiza ukweli katika kutoa taarifa kwa namna bora, kutumia lugha sahihi na kutatua changamoto kabla wengine hawajaziibua”Lakini lazima Mamlaka ya taasisi ishirikishwe”.
Aidha, katibu Mkuu huyo ametoa msisitizo kwa Maafisa Habari kwenda “field”kuona taasisi inatekeleza nini kwa wananchi ili atoe taarifa sahihi.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hosptali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Eligaesha alitoa pongezi kwa Katibu Mkuu huyo kwa namna alivyofanya mageuzi ya utoaji habari za Serikali kupitia vitengo vya mawasiliano.