Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Jenerali Gerald Kusaya akizungumza na waandishi wa habari katika semina iliyowahusisha waandishi iliyofanyika makao makuu ya mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa habari wakifuatilia mada zinazotolewa kuhusu kupambana na madawa ya kulevya katika semina ya waandishi wa habari iliyofanyika leo makao makuu ya mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO
Imeelezwa kuwa Tanzania imefanikiwa kwa Asilimia 90 kupambana na Wimbi la Madawa ya kulevya kutoka katika vyanzo vikuu vya kusambaza na kufanya Biashara hiyo.
Akizungumza leo na Wandishi wa habari katika jijini Dar es Salaam Kamishina wa kinga na tiba Dkt Peter Mfisi, amesema kuwa kwa Twakimu hizo ni kwa Mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC),
Amesema mafanikio hayo ni kutokana na jitihada zinazofanywa na mamlaka hiyo kwa kushirikia na vyombo mbalimbali vya serikali,Tasisi za Umma na zisizo za umma,Waandishi wa habaria pamoja na Wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevya Jenerali Gerald Kusaya amesema kuwa Vita Dhidi ya madawa ya kulevya ni muhimu ili kuimarisha nguvu kazi ambayo kwa kiasi kikubwa vijana wamekuwa Waraibu wa Tatizo hilo.
Naye Kaimu Kamishina wa kitengo cha huduma na Sheria Bi.Christina Rweshambura Ameelezwa baadhi ya adhabu na zilizobainishwa katika vifungu vya sheria ya kupambana na madawa ya kulevya moja ya adhabu hizo ni pamoja na atakaye kamatwa na madawa ya kulevya aina ya heroine na cocaine gramu 200 ni kifungo cha maisha.