…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu wawili kwa kufanya mauaji ya Samsoni Kikoti (56) kwa kutumia silaha aina ya Gobole pamoja na silaha mbili aina ya gobole zilizotumika katika mauaji hayo.
Hayo yamesemwa leo Mei 26,2021 jijini Dodoma na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto,amesema kuwa tukio hilo la mauaji limetokea katika kijiji cha Nhinhi Wilaya ya Chamwino ambapo watuhumiwa wawili Saimon Kikoti(36) na mwenzake George Mhando (44) walimuua mtu huyo.
Kamanda Muroto amesema kuwa baada ya kuhojiwa kwa watuhumiwa hao wamekiri kuhusika na katika mauaji kwa kutumia Silaha huku ikielezwa chanzo na sababu kujichukulia sharia mkononi kwa kumtuhumu Marehemu kuwa ni mwizi wan mifugo kwa muda mrefu.
“Watu waache kujichukulia sheria mkononi kama mtu anatuhumiwa kwa makosa ya uhalifu mtoe taarifa katika kituo cha polisi ili waweze kukamatwa na kufanyiwa uchunguzi dhidi ya makosa yao “amesema Kamanda Muroto.
Muroto amesema kuwa katika msako mwingine jeshi la polisi limewakata jumla ya watu 23 wakicheza kamali kinyume na sheria katika mitaa ya Bahi road na Makulu Tarafa na Wilaya ya Jiji la Dodoma .
Kuwa katika msako wa Tarehe 25 mwaka huu mtaa wa Amani kata ya Chang’ombe walikamatwa Maulid Shaka (33)mkazi wa chang’ombe na wenzake 6 wakijuhusisha na vitendo vya uhalifu wa uporaji kwa kutumia usafiri wa pikipiki tofauti.
“Watuhumiwa walikuwa wanatafutwa kwa makosa haya mbinu wanayotumia kupakia abiria nyakati za usiku na wengine wanawafuata nyuma na kuwavamia hukun wakiwapora wakati abiria anashushwa au akiwa njiani “amesema
“Wakati tukiendelea na msako kila sehemu tulifanikiwa kukamata Pikipiki mbili ambazo wamekuwa wakizitumia kufanyia uhalifu huo ambazo ni MC.601 BQL HAOJUE na MCL.154 CJJ BOXER “ amesema Muroto.
Aidha Jeshi hilo limekamata watuhumiwa mbalimbali waliojihusisha na vitendo vya madawa ya kulevya Gramu 2.8 ,bangi Gramu 15.4,na pombe haramu ya moshi inayojulikana kama Gongo lita 35 .
Hata hivyo Muroto ametoa wito kwa wale wote wanaojihusisha na kumiliki silaha kinyume na taratibu ,wauzaji na wasafirishaji wa madawa ya kulevya ,wanaopokea na kuhifadhi mali za wizi wajilasilimishe wenyewe huku akidai watakao kaidi agizo hilo hawatapona kwenye msako mkali unaoendelea.