MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amemaliza sitofahamu ya uongozi wa manispaa ilijitokeza Kati ya Meya manispaa ya kinondoni Songoro Mnyonge na Mkurugenzi wa Manispaa Spora Liana.
Utatuzi wa mgogoro huo umefanyika leo katika kikao cha pamoja kilichoitishwa leo na mkuu wa Mkoa na kuwakutanisha meya na mkurugenzi wa Manispaa ya kinondoni.
Makalla amewataka viongozi hao kurejea ofisini na kufanya kazi kwa pamoja, kutekeleza miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi.
Kwa upande wa Meya na mkurugenzi wamemaliza tofauti zao na wamehaidi kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya wananchi.