……………………………………………………………………………………………
Shirika la Raising up Friendship Foundation (RUFFO) pamoja na Kampuni ya KUKAJA kwa kushirikiana na wadau wameandaa kampeni ya SITANYAMAZA CHILDREN FUN RUN itakayofanyika tarehe 30/5/2021 jijini Dar es Salaam.
Lengo la kampeni hiyo ni kuwakutanisha watoto wote wa kike na wa kiume wenye umri kuanzia miaka 6 hadi 17 kwa ajili ya kupaza sauti zao na kuvunja ukimya watakapofanyiwa ukatili.
Kampeni ya SITANYAMAZA NITASEMA UKATILI UNAUA NDOTO ZA WATOTO ni sehemu ya jitihada za mashirika hayo katika kuhakikisha wanaendelea kutokomeza ukatili.
Mkurugenzi wa Shirika la Raising Up Friendship Foundation Bi. Hilda Ngoja amesema kuwa wazazi na walezi wametakiwa kuwashirikisha watoto wao kuhusu kusimamia ulinzi na usalama wao.
Ameeleza kuwa watoto wote wanakaribishwa kujiandikisha ili wapaze sauti zao kwa kujisajili kwa kila mshiriki kwa kupiga namba 0765670746 au 0629 848905.