TIMU ya Manchester City jana imeibuka na ushindi wa 4-3 dhidi ya wenyeji, Newcastle United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa St. James’ Park.
Mabao ya Man City ambao tayari ni mabingwa wa msimu yamefungwa naJoao Cancelo dakika ya 39 na Ferran Torres dakika ya 42, 64 na 66, wakati ya Newcastle yamefungwa na Emil Krafth dakika ya 25, Joelinton dakika ya 45 na ushei na Joseph Willock dakika ya 62.
Manchester City inafikisha pointi 83 baada ya ushindi huo katika mechi ya 36, ikiwazidi pointi 13 mahasimu wao, Manchester United, wakati Newcastle United yenyewe inabaki na pointi zake 39 za mechi 36 katika nafasi ya 16.