Katika kushereea Sikukuu ya Eid El Fitr Waumini wa dini ya Kiislamu mjini hapa wameshiriki Swala ya Eid iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye mkoani hapa ambapo walipata nafasi ya kusali kwa pamoja kumshukuru Mungu kwa kumaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani salama kama wanavyoonekana katika picha wakiswali.
Sheikh wa Kata ya Mungumaji Juma Sungi (katikati), akiongoza kuomba dua katika Swala hiyo. Kushoto ni Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Singida, Burhan Mlau. na kulia ni Qadhi wa Mkoa, Shaban Mkanga.
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Singida, Burhan Mlau. (kushoto) na Kaimu Sheik wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro wakiomba dua katika swala hiyo.
Waumini wa dini ya kiislamu wa mkoa wa Singida wakishiriki swala hiyo.
Waumini wa dini ya kiislamu wa mkoa wa Singida wakishiriki swala hiyo.
Swala ikiendelea.
Wanawake wa Kiislamu wakiwa kwenye swala hiyo.
Msomaji maarufu wa Qulaan hapa nchini, Ibrahim Mtigo akisoma Qulaan katika swala hiyo.
Mzee Hassan Mukhandi, akishiriki swala hiyo.
Dua ikifanyika.
Dua ikifanyika. kutoka kushoto ni Shabani Mswaki,Abrahman Masaka, Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Singida, Burhan Mlau. na Kaimu Sheik wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro.
Qadhi wa Mkoa wa Singida, Sheikh Shabani Mkanga akisoma hutuba katika swala hiyo..
|
Muumini wa dini hiyo, Barua Mwakilanga akizungumzia umuhimu wa swala hiyo ya Eid El Fitr |
Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu (Bakwata) Mkoa wa Singida, Burhan Mlau., akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kumalizika kwa swala hiyo.
Dua ikifanyika.
Baadhi ya Waislamu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya swala ya Eid El Fitr.
Dotto Mwaibale na Boniphace Jilili, Singida
KATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid El Fitr Waumini wa dini ya Kiislamu mjini hapa wameshiriki Swala ya Eid iliyofanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Sumaye ambapo walipata nafasi ya kusali kwa pamoja na kumshukuru Mungu kwa kumaliza Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani salama.
Akizungumza katika swala hiyo Kaimu Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Singida, Issa Nassoro aliwaomba waislamu kusherehekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu nakufuata maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine watakayoyatoa siku leo.
Katika hatua nyingine aliwataka waumini hao kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa Corona na kufuata maelekezo mbalimbali yanayotolewa na wataalamu wa afya.
Aidha Nassoro amewahimiza waumini hao kuwaenzi,kuwathamini, kutambua mchango wao na kuwatunza wajane wa viongozi wa dini hiyo na sii kuwafanyia hivyo pindi wawapo hai waume zao.
Akionyesha uzito na umuhimu wa jambo hilo Sheikh Nassoro alisema kuwa watatumia siku ya leo kwenda kuwatembelea wajane hao akiwemo mke wa aliyekuwa Sheikh wa Mkoa huo Salmu Mohamed Mahami ambaye alifariki hivi karibuni.
Kwa upande wake Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa huo Alhaji Burhan Mlau aliwaomba waislamu kusherehekea siku kuu hiyo kwa kufanya mambo mazuri kwani mwenyezi Mungu yupo siku zote na sio tu kipindi cha mfungo.
Aliwahimiza waumini hao pamoja na watoto wao kuacha tabia ya kwenda kwenye kumbi za starehe kufanya mambo yasiyompendeza Mungu na kwamba hayo sio maelekezo ya mwenyezi Mungu.
Mlau aliwataka waumini hao kupendana na kuwaomba wale wenye uwezo kuwasaidia wasio na uwezo kwa kuwapatia vitu mbalimbali ikiwemo chakula ili na wao wajione kuwa ni sehemu ya waliosherehekea sikukuu hiyo.