MBUNGE wa Jimbo la Kyela Mkoani Mbeya Ally Mlagila Jumbe akizungumza mbele ya wajumbe
MBUNGE wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya Ally Mlagila Jumbe akimtambulisha katibu Mohamed Mallavah
Baadhi ya wajumbe wa Ccm wilaya ya Kyela wakiwa katika mkutano.(picha na Denis Mlowe)
………………………………………………………………………………………..
DENIS MLOWE , KYELA
MBUNGE wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya Ally Mlagila Jumbe ametoa wito kwa wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa kuchagua mwenyekiti mpya wa wilaya ya Kyela CCM ambaye atawapeleka mbele zaidi katika kusimamia serikali.
Akizungumza wakati wa kujiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CCM wilaya ya Kyela, baada ya kuwa mbunge wa Jimbo hilo Kinanazi alisema kuwa kiongozi anayehitajika ni Yule ambaye Yuko tayari kusimamia misingi imara ya ccm na kuondoka na makundi.
“kiongozi ambaye anahitajika ni Yule ambaye hataturudisha nyuma kwenye makundi , kiongozi ambaye atasimamia imara usimamizi wa serikali hivyo wajumbe mtuletee huyo” alisema.
Alisema kuwa mwenyekiti atakayechaguliwa lazima awajibike kwa wanachama wa Ccm na sio Wanachama wawajibike kwake.
alisema kuwa mwenyekiti anayehitajika ajue umuhimu wa umoja wa mshikamano ndani ya chama, kama nguzo muhimu ya kufikia malengo na utekelezaji wa ilani ya chama chao.
Wajumbe walioshiriki kwenye mkutano mkuu wa wilaya na kupiga kura walikuwa 1259 ambapo wagombea waliojitokeza walikuwa watatu.
Kwa Upande wake Katibu Mwenezi CCM wa wilaya Kyela , Emanuel Kiketelo Mwamulinge alisema kuwa maandalizi ya uchaguzi yameandaliwa vyema na wajumbe wamejitokeza kwa wingi.
Kama Mwenezi Nina na wajumbe watatuletea mwenyekiti mwenye uwezo mkubwa na ushawishi kwenye chama na jamii katika kuisimamia serikali.