Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akizungumza katika hafla ya siku ya wanafunzi ya ubunifu na ujasiriamali na fainali za shindano la mwaka la ubunifu na ujasiriamali la Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) yaliyofanyika Chuoni hapo leo Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo akitazama bidhaa zilizotengenezwa na wajasiriamali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika hafla ya siku ya wanafunzi ya ubunifu na ujasiriamali na fainali za shindano la mwaka la ubunifu na ujasiriamali la Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) yaliyofanyika Chuoni hapo leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Prof. william Anangisye akizungumza katika hafla ya siku ya wanafunzi ya ubunifu na ujasiriamali na fainali za shindano la mwaka la ubunifu na ujasiriamali la Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) yaliyofanyika Chuoni hapo leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya siku ya wanafunzi ya ubunifu na ujasiriamali na fainali za shindano la mwaka la ubunifu na ujasiriamali la Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) yaliyofanyika Chuoni hapo leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO
*******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo ameupongeza uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa na vitengo mbalimbali vinavyosimamia wanafunzi wajasiriamali ambao unawajengea nafasi kubwa ya kujiajiri pindi wakimaliza masomo yao chuoni.
Akizungumza katika hafla ya siku ya wanafunzi ya ubunifu na ujasiriamali, na fainali ya shindano la ubunifu na ujasiriamali Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika ukumbi wa Nkrumah Prof.Mkumbo amesema kuwa swala la kukosa ubunifu kwa vijana hasa wahitimu limechangia kwa kiwango kikubwa kubakia na matatizo mengi katika jamii zetu na jamii kutoona faida za wasomi katika taifa hili.
“Utafiti umeonyesha kwamba unapochanganya watu wa fani tofauti, jinsia tofauti, tamaduni tofauti na mawazo tofauti kujifunza pamoja inaibua ubunifu wa kiwango cha juu”. Amesema Prof.Mkumbo.
Aidha Prof.Mkumbo amewasihi wajasiriamali kujifunza lugha ya kiingereza kwa maana ujasirimali mkubwa unaji lugha ya kiingereza ili kuweza kuwafikia watu wengi ulimwenguni.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. william Anangisye amesema kuwa kutokana na ongezeko la wahitimu katika soko la ajira na changamoto ya sasa ya ajira, Chuo Kikuu kinatilia mkazo elimu ya ubunifu na ujasiriamali katika fani zote za masomo.
“Chuo Kikuu kimejipanga kimkakati kufanya mabadiliko katika mitaala yake ili kutoa elimu ambayo itawafanya wahitimu wake wakidhi vigezo vya soko la ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri”. Amesema Prof.Anangisye.
Pamoja na hayo Prof.Anangisye amesema kuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kina vitengo vinavyosaidia wabunifu na wajasiriamali kuendeleza mawazo yao ya kibunifu/kijasiriamali.
“Vitengo hivi ni pamoja na Kurugenzi ya Ubunifu na Ujasiriamali (UDIEC), ambayo huratibu shughuli zote za mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali hapa chuoni ambazo haziko katika mitaala, kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanataaluma ili waweze kufundisha masomo ya ubunifu na ujasiriamali katika vitengo vyao; na kukiunganisha CKD na wadau wa nje katika masuala ya ubunifu na ujasiriamali”. Amesema Prof.Anangisye.
Hata hivyo Prof.Anangisye amesema kuwa Chuo kimetenga bajeti ya kila mwaka kuendesha mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu katika mikoa mingi ya hapa nchini.