BAADHI ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hafla ya kukabidhi Mpango wa Ujenzi wa Bandari ya Mwangapwani Zanzibar (Master Plan) ukiwasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman Bw.Mohamed Al Tooqi.(hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 7-5-2021.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman Bw. Mohamed Al Tooqi akiwasilisha Mpango wa Ujenzi wa Bandari ya Mwangapwani Zanzibar (Master Plan) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akikabidhi Mpango wa Ujenzi wa Bandari ya Mwangapwani Zanzibar (Master Plan) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman Bw. Mohamed Al Tooqi, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza wakati wa kukabidhiwa Mpango wa Ujenzi wa Bandari ya Mwangapwani Zanzibar (Master Plan) uliotayarishwa na Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
KATIBU wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Dkt.Mwinyi Talib Haji, Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar.Mhe Rahma Kassim Ali na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mpango wa Ujenzi wa Bandari ya Mwangapwani Zanzibar.(Master Plan) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)