Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara akifungua akifungua mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2021.
Wakandarasi waliohudhuria mkutano huo
**************************
NANAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Mwita Waitara ameipongeza bodi ya usajili makandarasi kwa kuboresha mfuko wa kuwasaidia makandarasi kwa kutoa thamana milioni 100 kwenda bilioni 50 kama ilivyokuwa awali bila kujali daraja usajili.
Mhe Waitara alitoa pongezi hizo wakati akifungua mkutano wa mashauriano na wadau wa sekta ya ujenzi kwa mwaka 2021 ambapo alisema kuwa kutokana na hilo wizara itaendelea kushirikiana na bodi hiyo ikiwa ni pamoja kuendelea kuhakikisha miradi isiyodhidi bilioni 10 inatekelezwa na makandarasi wa ndani.
Aliwaeleza kuwa wanapaswa kuungana na kufunga mkanda wanapopata miradi kwa kuwa waaminifu na kuhakikisha wanatekeleza kwa wakati pamoja na kuakisi thamani halisi ya fedha kwani kwa upande wa serikali hawana shida hivyo waweke mambo yao vizuri.
“Hatuna shida na usomi wa makandarasi watanzania ila kuna mambo madogodogo mnapaswa kuyaangalia kwani sio malengo ya serikali kukupa kazi alafu badala ya kufanya kazi hiyo na kutekeleza kwa wakati unaenda kufanya mambo mengine na mwisho wa siku mradi unakwama,”Alisema Mhe Waitara.
Aidha kuhusiana suala la utekelezaji miradi ya serikali kwa kutumia Force akaunti ambayo inawanyima fursa makandarasi kupata kazi alisema kuwa majibu ya suala hilo watalipata rasmi katika mkutano unaofuata utakaofanyika Mwanza kutoka kwa waziri mwenye dhamana Mhandisi Leonard Chumuriho.
Alifafanua kuwa Force akaunti ni kwaajili ya kupunguza gharama na kupata matokeo ya haraka lakini kama wamepunguza gharama na kuendana na hali halisi ya uchumi wa nchi jambo hilo linazungumzika kwani wanaamini katika utaalamu lakini tatizo linakuja katika changamoto ya kimahitaji yaliyopo katika nchi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya makandarasi Cosolata Ngimbwa hali ya wakandarasi kiuchumi kwa sasa ni mbaya na yote ni kutokana na serikali kuamua kuamua kutumia Force akaunti ambapo ameiomba serikali kuwapa nafasi makandarasi kwani wameiva na watajenga katika ubora unahitajika na kwa wakati.
“Tamisemi wana kazi nyingi lakini wamewapa local fundi sasa tunaomba wapeni makandarasi hawa kwani wamejifunza na watafanya kwa bei nzuri na kumaliza,” Alisema Cosolata.
Sambamba na hayo aliwataka makandarasi kuacha makundi bali wawe na sauti moja ambayo itawafanya wakae chini na kuzungumza na serikali na sio kila mtu kuongea kivyake kwani hawataweza wala hawataingia katika miradi hiyo.
Naye msajili wa bodi hiyo Mhandisi Rhoben Nkori alisema kuwa kwa mwaka 2020 wameweza kuwasajili makandarasi 907 na kufanya jumla ya makandarasi waliosajiliwa kuwa 11749 pamoja na kusajili miradi 3179 ya ujezi yenye thamani ya shiliomgi trilioni 3.8 huku asilimia 96.7 ikiwa imefanywa na makandarasi wa ndani na asiliia 3.3 ikifanywa tna maandarasi wa nje.
Alifafanua kuwa miradi asilimia 96.7 ilikuwa na thmani ya asilimia 46.5 ikilinganishwa na miradi asilimia 3.3 iliyofanywa na wageni kuwa na thamani ya asilimia 53.3.