Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi, wakionesha mfano wa fulana mojawapo kati ya mia nne (400) zilizokabidhiwa na NMB zitakazotumika katika Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku kuanzia tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021 yaliyobeba kauli mbiu isemayo “SHULE ZETU NI CHANZO CHA MAARIFA TUZILINDE DHIDI YA MAJANGA YA MOTO”. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jjijini Dodoma, Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (Wapili kulia) akimkabidhi baadhi ya Vifaa vya michezo Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza (Wapili kushoto), vilivyotolewa na NMB vitakavyotumika katika Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku kuanzia tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021 yaliyobeba kauli mbiu isemayo “SHULE ZETU NI CHANZO CHA MAARIFA TUZILINDE DHIDI YA MAJANGA YA MOTO”. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jjijini Dodoma, Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Sehemu ya Maofisa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, pamoja na Maofisa wa Benki ya NMB wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya vifaa hivyo.
Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza (Wapili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi (Wapili kulia) na baadhi ya Maofisa wa Benki ya NMB pamoja na wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mara baada ya zoezi la kukabidhiwa Vifaa mbalimbali vya michezo pamoja na fulana zitakazotumika katika Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku kuanzia tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021 yaliyobeba kauli mbiu isemayo “SHULE ZETU NI CHANZO CHA MAARIFA TUZILINDE DHIDI YA MAJANGA YA MOTO”. Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jjijini Dodoma, Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. (Picha Zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
………………………………………………………………………….
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepokea msaada wa Vifaa mbalimbali vya michezo pamoja na fulana vitakavyotumika katika Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku kuanzia tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021 ambayo yatashirikisha Taasisi za Serikali na binafsi.
Vifaa hivyo ni pamoja na mipira kumi (10) kwa ajili ya michezo mbalimbali, fulana mia nne (400) na Vikombe vitatu (3) vitakavyogawiwa kwa washindi wakati wa Maadhimisho hayo, vilikabidhiwa na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati Nsolo Mlozi kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Vifaa hivyo leo jijini Dodoma, bwana Mlozi amesema NMB inatambua mchango wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Kuokoa Maisha na Mali za Watanzania, msaada huu utakuwa chachu katika kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa inayotarajia kuanza hivi karibuni.
Bwana Mlozi amelishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia kwa Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo Mbaraka Semwanza kwa niaba ya Kamishna Jenerali kwa huduma wanazozitoa kwa jamii na kuhakikisha Maisha na mali za Watanzania vinakuwa salama na kuahidi kuendelea kushirikiana kwa dhati.
Akiongea baada ya kupokea vifaa hivyo, Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza ameshukuru kwa msaada na kusema kuwa utaongeza chachu katika kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yatakayofanyika Mkoani Morogoro katika Viwanja vya Tumbaku kuanzia tarehe 17 Mei hadi 21 Mei, 2021.
“Tunawashukuru sana NMB, benki hii imekuwa mshirika wetu mkubwa sana katika nyanja mbalimbali, msaada huu tutautumia vyema katika kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa iliyopo mbele yetu inayotarajia kuanza hivi karibuni” Alisema Kamishna Semwanza.
Aidha Kamishna Semwanza ametoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Morogoro pamoja na Wilaya zake na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika Viwanja vya Tumbako ambako Maadhimisho hayo yatafanyika yaliyobeba kauli mbiu isemayo “SHULE ZETU NI CHANZO CHA MAARIFA TUZILINDE DHIDI YA MAJANGA YA MOTO”.