RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa Mei 07 anatarajiwa kufanya mkutano na zaidi ya Wazee 900 wa Mkoa wa Dar es salaam ambapo Katika kikao hicho watajadili mambo mbalimbali.
Akitoa taarifa ya Mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema kikao icho kitafanyika Ukumbi wa Mikutano Mlimani city kuanzia saa 8 Mchana.
Aidha RC Kunenge ametoa wito kwa Wazee waliopata mialiko ya kushiriki kikaoh icho kujitokeza kwa wingi ili wapate kusikiliza kile ambacho Rais Mhe. Samia amewaitia.
Kwa upande wao Viongozi wa Wazee wamemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kuona umuhimu wa kukutana na Wazee huku wakisema wanatarajia Kikao hicho kitakuwa na Manufaa makubwa kwao.