**********************
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Iddi Hassan Kimanta amezindua nyumba mpya ya walimu (two in one) yenye vyumba sita na huduma zote muhimu ndani ikiwa ni sehemu ya ukamilishaji wa ujenzi wa shule ya Msingi mpya ya Kerikeny kata ya shambarai Burka Halmashauri ya meru
Katika ziara hiyo Mhe Kimanta alipokea taarifa ya ujenzi wa shule hiyo kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Jerry Muro ambapo amesema kwa sasa miundombinu ya shule imekamilika kutokana na kukamilika pia ujenzi wa vyoo vipya na vya kisasa vyenye matundu 20 ambapo kati ya hayo kumi ni wavulana na kumi ni wasichana
Kutokana na kuridhishwa na ujenzi huo, Mhe Kimanta ametoa matofali 1,500 kwa ajili ya kukamilisha jengo jipya la ofisi za mwalimu mkuu pamoja na walimu uku Mkuu wa wilaya ya Arumeru Ndugu Muro akitoa mifuko 30 ya saruji na mkurugenzi wa Halmashauri ya meru Ndugu Emmanuel Mkongo pamoja na mwenyekiti wa Halmashauri Ndugu kishili wakihaidi kumalizia jengo hilo kwa kuezeka na finishing ya mwisho.