Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa NHC,Itandula Gambalagi ,akiwaeleza waandishi wa habari jinsi ujenzi wa nyumba hizo unaenda kwa kasi ili kuhakikisha ifikapo Julai zinaanza kutumika na wakati wa kukagua maeneo zinapojengwa nyumba hizo Chamwino na Iyumbu ziara iliyofanyika leo Mei 5,2021.
Mhandisi anayesimamia Ujenzi wa nyumba Chamwino Grace Msita,akizungumzia nyumba hizo zinajengwa katika ubora wa hali ya juu ambapo madini ya ujenzi kama kokoto, mawe na mchanga vinapimwa ubora wake katika maabara ya Tarura kabla ya kutumika wakati wa kukagua ujenzi wa nyumba zinazojengwa Chamwino Mkoani Dodoma ziara iliyofanyika leo Mei 5,2021.
Meneja Mradi wa Nyumba 1000 Dodoma,Frank Mambo,akielezea ubora wa majengo unapimwa na taasisi zinazohusika na viwango, na hadi sasa ujenzi umefikia asimilia kati ya 35 na 40 kwa Chamwino na 40 kwa Iyumbu wakati wa kukagua maeneo zinapojengwa nyumba hizo Chamwino na Iyumbu ziara iliyofanyika leo Mei 5,2021.
Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa NHC,Itandula Gambalagi ,akiwaonyesha ramani ya muonekano wa nyumba waandishi wa habari (hawapo pichani) zinazojengwa Chamwino wakati wa ziara iliyofanyika leo Mei 5,2021.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Dk.Maulidi Banyani,akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) ujenzi wa nyumba za NHC zinazojengwa Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma mara baada ya kufanya ziara ya kukagua na kutembelea maeneo zinapojengwa nyumba hizo Chamwino na Iyumbu leo Mei 5,2021.
Mkurugenzi wa Uhandisi na Ujenzi wa NHC, Haikamen Mlekio akizungumzia jinsi walivyojiongeza katika maeneo yote mawili Chamwino na Iyumbu kwa kununua mashine 17 za kutengeneza matofali ambazo zimeajiri vijana 60 ambao wana uwezo wa kutengeneza matofali 20,000 kwa siku wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maeneo zinapojengwa nyumba hizo Chamwino na Iyumbu iliyofanyika leo Mei 5,2021.
Mafundi wakiendelea na kasi ya ujenzi wa nyumba za NHC zinazojengwa Chamwino.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Dk.Maulidi Banyani,akielezea jambo kwa waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo la ujenzi wa nyumba za NHC zinazojengwa Iyumbu wakati wa kukagua na kutembelea maeneo ya Chamwino na Iyumbu ziara iliyofanyika leo Mei 5,2021.
Muonekano wa nyumba zinazojengwa Iyumbu.
…………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Dk. Banyani amesema mradi huu unajengwa kwa msaada wa Serikali ambayo iliikopesha Shirika hilo mkopo nafuu wa Sh Bilioni 20 huku wao wakitoa Sh Bilioni 1.4 na kufanya jumla ya gharama ya mradi huo kuwa Sh Bilioni 21.4.
” Tunashukuru kwa mkopo huu ambao tumepewa na serikali yetu ambao ni nafuu, mpaka sasa mradi wa nyumba za Chamwino umefikia asilimia 35 na unaelekea asilimia 40 na mradi wa Iyumbu wa nyumba 300 ukiwa umefikia asilimia 40, miradi yote hii ipo ndani ya wakati na tunaamini kufikia mwezi Juni tutaanza mchakato wetu wa mauzo.
Awamu hii nyumba zetu tumezingatia ubora wa ujenzi, ukubwa wa nyumba na eneo pamoja na uzuri wa majengo, vitu hivyo vimechangia kwa kiasi kikubwa mwamko wa wateja kuwa mkubwa na tunaamini tukitangaza rasmi mauzo tutapata wateja wengi sana,” Amesema Dk Banyani.
Amesema katika nyumba 300 za Iyumbu ambazo zitauzwa bei yake itakua Sh Milioni 50-99 kulingana na ukubwa wa nyumba na eneo huku pia kukiwa na maeneo ya kupumzikia, maeneo ya Biashara, viwanja vya michezo na Shule ya awali.
” Ununuaji wa nyumba hizi unamlenga kila mtanzania yeyote, kama mtu ataamua kulipa papo kwa papo ni sawa kama ataamua kukopa pia tutamuuzia kwa makubaliano na benki ambayo amekubaliana nayo, niwasihi watanzania wa Dodoma kuchangamkia nyumba hizi zinazojengwa na Shirika lao.
Malengo yetu siyo kuishia Iyumbu na Chamwino tu, tutafikia maeneo tofauti ndani ya Mkoa huu, na pia tumejipanga kuyafikia maeneo yote ya Nchi yetu, Mkoa kwa Mkoa hadi ngazi za Wilaya, kiu yetu ni kujenga nyumba bora za Kisasa kwa ajili ya Watanzania, ” Amesisitiza Dk Banyani.
Hata hivyo Dk.Banyani amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa watu wanaonunua nyumba Iyumbu wanapata huduma stahili bila kufuata mjini kilometa 15 hivi, pia shirika hilo litajenga maduka ya biashara, shule ya awali, maduka na ofisi na baadaye makao makuu ya shirika.
Awali Kaimu Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa NHC,Itandula Gambalagi amesema kuwa ujenzi wa nyumba hizo unaenda kwa kasi ili kuhakikisha ifikapo Julai zinaanza kutumika na hivyo kupunguza tatizo la upungufu wa nyumba kwa watumishi jijini humo.
Naye Mhandisi anayesimamia Ujenzi wa nyumba Chamwino Grace Msita amesema kuwa, nyumba hizo zinajengwa katika ubora wa hali ya juu ambapo madini ya ujenzi kama kokoto, mawe na mchanga vinapimwa ubora wake katika maabara ya Tarura kabla ya kutumika.
Meneja Mradi wa Nyumba 1000 Dodoma,Frank Mambo, amesema ubora wa majengo unapimwa na taasisi zinazohusika na viwango, na hadi sasa ujenzi umefikia asimilia kati ya 35 na 40 kwa Chamwino na 40 kwa Iyumbu.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhandisi na Ujenzi wa NHC, Haikamen Mlekio amesema kuwa kampuni imejiongeza katika maeneo yote mawili Chamwino na Iyumbu kwa kununua mashine 17 za kutengeneza matofali ambazo zimeajiri vijana 60 ambao wana uwezo wa kutengeneza matofali 20,000 kwa siku, kitendo hicho kimeimarisha ubora wa mayofali, kupunguza gharama zilizokuwa zikitumika kutokana kuagiza kwa watu.“Shirila hilo kwa kujenga nyumba hizo limeajiri jumla ya vijana 450 kwa kuzingatia jinsi kwani limeajiri wanawake asilimia 40 na wanaume asilimia 60 pia limeajiri wenye ulemavu wawili.