Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika maandamano ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza meza kuu kushuhudia maandamano ya Watumishi wa Umma na binafsi waliokuwa wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa kilele cha siku ya wafanyakazi duniani (hawapo pichani) iliyoadhimishwa kitaifa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Liberata Mulamula (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika jijini Mwanza katika uwanja wa CCM Kirumba.
Sehemu ya Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakifuatilia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa jijini Mwanza
Sehemu ya Mawaziri wa Wizara mbalimbali na Wakuu wa taasisi mbalimbali wakifuatilia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.
*******************
Na Mwandishi wetu, Mwanza
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imeungana na Wizara, Taasisi, Mashirika na Kampuni binafsi katika kushiriki maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Mwanza.
Maadhimisho hayo yameongwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiambatana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Husein Kattanga, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb), Mawaziri wa wizara mbalimbali pamoja na Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameongozwa na Waziri wake Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb), Naibu Waziri Mhe. Balozi Mbarouk Nassoro Mbarouk (Mb) pamoja na Katibu Mkuu Mhe. Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
Kaulimbiu katika maadhimisho hayo ni Maslahi bora, Mishahara juu, Kazi iendelee.