***********
Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa Tarafa wa Mihambwe Ndg.Emmanuel Shilatu ametembelea Maghala ya vyama vya msingi yanayopokea ufuta kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani ya Mihambwe na Michenjele yaliyopo Tarafa ya Mihambwe ili kujionea utaratibu unaotumika.
“Kazi ya Serikali ni kuwasimamia, kuona mambo yanaenda vyema. Nimekuja kuwatembelea ili kuona changamoto zilizopo ili kuzitatua na pia kujiridhisha na utaratibu unaotumika. Kwa taarifa mlizonipatia mnakiri malipo yanaenda vyema kwa ufuta uliouzwa tayari. Kwa upande wa Mnunuzi ajitahidi sana kuja kuuchukua mzigo wake kwa wakati mara tu afanyapo malipo”. Alisisitiza Gavana Shilatu.
Wakulima wanaendelea kujitokeza kwa wingi kuleta ufuta ghalani na hadi sasa minada minne mikubwa imefanyika ya kuuza ufuta ambapo 60% ya makusanyo yote mpaka sasa yameshauzwa na Wakulima wameshalipwa fedha zao.