Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara zenye dhamana yaElimu,Michezo na
TAMISEMI wakiwa kwenye kikao kazi leo Aprili 27,2021 Jijini Dodoma
kujadili utekelezaji wa maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana hizo hizo kwa lengo la
kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa masuala mbalimbali ya
uimarishaji wa somo la
Elimu kwa Michezo na Michezo katika shule za Msingi na Sekondari hapa
nchini chini ya uenyekiti wa Prof.Riziki Shemdoe ambaye ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya
TAMISEMI.
Dkt. Hasssan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI anayeshughulikia eneo
la Elimu ndugu Gerard Mweli (kulia)
wakihudhuria kikao cha Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara zenye dhamana ya Elimu,
Michezo na TAMISEMI
wamefanya kikao kazi leoAprili 27,2021Jijini Dodoma
kujadili utekelezaji wa maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana hizo hizo kwa lengo la
kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa masuala mbalimbali yauimarishaji wa somo la
Elimu kwa Michezo na Michezo katika shule za Msingi na Sekondari hapa nchini.
Upande wa pili ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusufu Omary Singo
Na John Mapepele, Dodoma
Kamati ya Makatibu Wakuu wa Wizara
zenye dhamana ya Elimu, Michezo na
TAMISEMI wamefanya kikao kazi leo Aprili
27,2021 Jijini Dodoma kujadili utekelezaji
wa maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana
hizo hizo kwa lengo la kuandaa Mkakati
wa Utekelezaji wa masuala
mbalimbali ya uimarishaji wa somo
la Elimu kwa Michezo na Michezo katika shule za Msingi na Sekondari hapa nchini
Mwenyekiti wa Kikao hicho, Prof.
Riziki Shemdoe ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI
amesema miongoni mwa mambo
yaliyojadiliwa na kukamilika ni pamoja
na kuandaliwa kwa mapendekezo ya uimarishaji wa ufundishaji wa
somo la michezo shuleni na tahasusi zenye somo hilo kwa kidato cha tano ambapo ameseme tahasusi hizo zitaanza
kufundishwa katika mwaka huu wa masomo.
Pia rasimu ya Mpango Mkakati na Mikakati
ya utekelezaji wa masuala mbalimbali ya
somo la Elimu kwa michezo na
michezo katika shule za Msingi na Sekondari
imeandaliwa ili kuboresha michezo mashuleni.
Kuhusu kuandaa kiunzi cha uendeshaji
wa michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA Prof. Shemdoe amesema tayari
Kamati ya Wataalam imeshauri kuwa kwa sasa
miongozo iliyopo itumike na kiunzi tayari kimeshaandaliwa kwa kuzingatia
changamoto zilizopo ambapo kitajadiliwa
na wadau wote Juni mwaka huu wakati wa michezo ya UMISHUMTA NA UMISSETA
na kwa sasa tayari miongozo hiyo
imeshatumwa kwenye mikoa yote hapa
nchini.
Aidha, suala la uundwaji wa Kamati ya
kitaifa ya UMISHUMTA NA UMISSETA tayari imependekezwa na kukubalika kuundwa kwa
Kamati ya Usimamizi itakayoundwa na wataalam wawili wawili kutoka kwenye kila
Wizara ambapo imekubalika kuwa pamoja na
usimamizi, Kamati itatumia fursa hiyo kujifunza na kuangalia changamoto
zilizopo kwenye uendeshaji wa michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA kuandaa mapendekezo yatakayojadiliwa na wadau wote kwa ajili ya maboresho zaidi.
Prof. Shemdoe amesema kuhusu mchakato
wa maandalizi ya UMISHUMTA NA UMISSETA mwaka huu, tayari mikoa yote
imeshaandikiwa barua ya taarifa na Mhe. Waziri Ofisi ya Rais –TAMISEMI na
kwamba waratibu wa michezo wanakwenda kwenye ukaguzi wa viwanja na maeneo ya malazi
na chakula kuanzia Aprili 28-30, mwaka huu. Pia Kamati ya wataalam inaendelea
na ufuatiliaji wa Shule teule za michezo ili kuhakikisha kuwa michezo
inafanyika kwenye kiwango kinachotakiwa.
Makatibu Wakuu walioshiriki kwenye
kikao hiki ni pamoja Mwenyekiti wa kikao hicho, Prof. Riziki Shemdoe ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI,na
Naibu wake anayeshughulikia eneo la
Elimu ndugu Gerard Mweli, mwingine ni Dkt. Hasssan Abbasi, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, na Dkt. Leonard Akwilapo kutoka
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojioa pamoja na Watendaji mbalimbali
kutoka Wizara hizo.
Maelekezo ya Mawaziri wenye dhamana ya elimu, Michezo
na TAMISEMI yalitolewa wakati wa kikao cha pamoja kilichofanyika Februari 8,
Mwaka huu.