*******************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi amesema kuwa hadi mwishoni mwa mwaka huu wa 2021 maeneo yenye changamoto ya umeme katika wilaya hiyo yatapata suluhu kikubwa ni wananchi kuwa na subira pamoja na kudumisha amani na utulivu.
Kenan aliyasema hayo wakati akiongea na wananchi wa baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo katika ziara ya kutembelea miradi ya umeme inayotekelezwa na shirika la umeme Tanzania (TANESCO) ambapo alisema kuwa kwa jiji la Arussha shirika hilo linajitahidi na kwa maeneo ambayo bado hawajafikiwa baada ya mwaka mpya wa fedha zoezi litaendelea.
“TANESCO kwa jinsi nilivyotembelea miradi hii na kujionea yanayoendelea kwa jiji la Arusha kweli wanahitaji na wametupendelea ninacho waomba wananchi ni muwe na subira na mwisho wa siku tuweze kuleta maendeleo kwa pamoja,”Alisema Kenan.
Alifafanua kuwa bado kuna changamoto ikiwemo baadhi ya maeneo ya Mkonoo, Erangau, Bondeni, Terrat, Muriet ambayo wananchi wameyaainisha lakini kwanzia mwezi wa saba changamoto hizo zitatatuliwa na shida ya ufungaji wa umeme itaondoka kabisa katika wilaya hiyo.
Kwamujibu wa taarifa ya TANESCO iliyosomwa na kaimu meneja wa shirirka hilo mhandisi Triphonia Massawe alisema kuwar hadi kufikia Januari 31,2021 jumla ya miradi 45 mipya yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.7imefunguliwa na inaendelea kutekelezwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Arusha.
“Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 tumeendelea na miradi hii mipya ya umeme kwa wananchi wa jiji la Arusha ili kuhakikisha ili kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na miundombinu ya nguzo karibu na nyumba yake ili aweze kulipia ndogo na nafuu ya umeme,”Alieleza Mhandisi Triphonia.
Alifafanua kuwa shirika hilo limejipanga kusambaza miundombinu ya umeme hasa maeneo ambayo yanaendea kukua kwa kasi ikiwemo eneo la barabara ya Afika Mashariki (By_Pass) kwa kuwa maeneo hayo yanakuwa KWA kasi kubwa lakini miundombinu ya umeme ipo mbali na makazi ya wananchi.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wakiwemo wa mtaa wa Engavmet kata ya Terrat wamesahaulika kwani katika eneo lao hakuna nguzo zilizosambazwa japo waliahidiwa kuwa hadi februari watakuwa wameshafikishiwa huduma hiyo ikiwa ni pamoja na wananchi wa maeneo mengine kulalamikia fedha wanayotozwa wakati wa uchoraji wa ramani ambapo utozwaji unatofautiana kutoka elfu 15 hadi 30.