Timu ya Azam FC imelipa kisasi cha kufungwa na Yanga mzunguko wa Kwanza baada ya leo kupata ushindi wa bao 1-0 mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
Shujaa wa Azam FC ni Mshambuliaji hatari Prince Dube aliyewanyanyua mashabiki wa Chamazi dakika ya 86 kwa shuti kali lililomshinda Farouk Shikalo.
Licha ya kufungwa Yanga wanabaki nafasi ya pili wakiwa na Pointi 57 huku Azam FC wakibaki nafasi ya tatu kwa Pointi 54.