**********************************
Mtendaji Mkuu (CEO), Barbara Gonzalez ameitangaza kampuni ya Vunja Bei kuwa mshindi wa tenda ya jezi za Simba.
Kwa mujibu wa Barbara mkataba wa tenda hiyo unagharimu shilingi bilioni mbili na ni wa miaka miwili.
Hata hivyo Msanii wa bongo fleva ambaye ni Mbunge wa zamani wa Mikumi Prof.Jay amesema jambo ambalo linafanywa na viongozi wa Simba ni zuri na lenye manufaa kwa wachezaji na wanasimba kwa ujumla.
“Simba imeonyesha mfano wa kuwaamini vijana wa Kitanzania na kuwapa dhamana kubwa kwa sababu wanaamini vijana kwenda kuleta mabadiliko.”- Profesa Jay.