Na Woinde Shizza, ARUSHA
Meneja wa shirika la Sido mkoa wa Arusha Nina Nchimbi amewataka vijana kubeba fursa zilizopo katika sekta ya utalii ili waweze kujiajiri na kuongeza mapato ya Taifa.
Aliyasema hayo jana wakati akiongea na vijana kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini waliouthuria kongamano la vijana la kujadili wajibu wakijana katika kudumisha amani lililoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali la PPVO lililofanyika mkoani hapa.
Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa hawajui zaidi kuhusu umuhimu wa wao kutembelea vivutio vyetu na suala zima la kukuza utalii wa ndani huku wengi wakionesha kutohamasika kutembelea vivutio hivyo iwapo kijana ataamua kutumia fursa kama hii na kuanza kuamasisha na kuwaelimisha umuhimu wakutembelea hifadhi zetu atakuwa amejitengenezea ajira kwani pindi watakapo safari atajiingizia fedha .
Alisema kuwa Tanzania ni nchi iliyojaliwa kuwa na vivutio vingi vya kuvutia kushinda nchi nyingine duniani,vivutio hivyo nikama vifuatavyo,mbuga za wanyama ambazo zipo 16,hifadhiza za taifa,malikale za taifa,Fukwe,Milima,Makumbusho ya Taifa,Vijiji vya makumbusho ,Ngoma za kitamaduni, Nasehemu za kihistoria kama Kalenga Iringa,Ngorongoro, na michoro ya mapangoni Kondoa Irangi.
Vivutio kama vivutio vipo vya kutosha ,ila kinacho hitajika ni serekali yetu kutoa fursa nyingi kwa watanzania kuweza kuvitangaza zaidi na kuhamasisha watalii wa ndani na waweze kwenda kuvitembelea kwa ajili mbalimbali ,serekali yetu inajukumu kubwa sana lakujenga miundo mbinu mbalimbali katika vivutio hivi.
Alisema kuwa vijana wanaweza kujiajiri kupitia maduka mbalimbali ya vinyago,vifaa vya kitamaduni na mavazi ya kitamaduni nimuhimu wakafunguwa katika sehemu mbalimbali ya nchi hii itawaongezea kujiajiri pia kwani , maduka haya yatawavutia watalii wengi wakigeni pamoja na wazawa kuja kutembelea vivutio vyetu na kununua vitu mbalimbali kamazawadi za kuwapelekea ndugu na marafiki zao huko walipotoka.
Aidha alisema kuwa ni vyema pia vijana wakatumia utalii kufungua vituo vya buradani za kitamaduni ndani ya hifadhi , kama vile ngoma za kimasai,na ngoma mbalimbali ambazo zitatoa burudani nzuri,mashindano mbalimbali kama mpira wa miguu wa ufukweni,(soccer beach) vitakuwa ni vivutio vizuri kwa wageni mbalimbali , kufika katika vivutio vyetu .
Akizungumza kwa niaba ya vijana walioshiriki kongamano hilo mwenyekiti wa bunge la vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jems Leornard amesema kuwa kupitia warsha hiyo anaamini kuwa vijana huko mbeleni watanufaika na fursa za utalii wa ndani.