Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Abdulmajid Nsekela (Kulia) akipokea cheti kutoka kwa Waziri Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mh. Mudrik Soraga Mara baada ya kuhitimishwa Mafunzo ya Siku tano yenye kulenga Uzalendo na Usalama wa Taifa katika Uwekezaji kwa Viongozi yaliyofanyika Chuo cha Ulinzi cha Taifa NDC Mwishoni mwa Wiki Jijini Dar es Salaam. PICHA NA KAPTENI SELEMANI SEMUNYU -JWTZ NDC.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMA -JKT Brigedia Jenerali Rajabu Mabele (Kulia) akipokea cheti kutoka kwa Waziri Ofisi ya Rais Kaz, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mh. Mudrik Soraga Mara baada ya kuhitimishwa Mafunzo ya Siku tano yenye kulenga uzalendo na Usalama wa Taifa katika Uwekezaji yaliyofanyika Chuo cha Ulinzi cha Taifa NDC Mwishoni mwa Wiki Jijini Dar es Salaam. PICHA NA KAPTENI SELEMANI SEMUNYU -JWTZ NDC
Mkuu wa Wilaya Pangani Zainab Abdalah (Kulia) akipokea cheti kutoka kwa Waziri Ofisi ya Rais Kazi,Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mh. Mudrik Soraga Mara baada ya kuhitimishwa Mafunzo ya Siku tano yenye kulenga Uzalendo na Usalama wa Taifa katika Uwekezaji kwa viongozi yaliyofanyika Chuo cha Ulinzi cha Taifa NDC Mwishoni mwa Wiki Jijini Dar es Salaam. PICHA NA KAPTENI SELEMANI SEMUNYU -JWTZ NDC.
****************************
Alisema hayo Mwishoni mwa Wiki wakati wa kufunga Mafunzo Maalum kozi fupi (Capstone)kundi la Kumi 2021 inayotolewa na Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi Nchini NDC kutoka Sekta binafsi na sekta za Umma yenye lengo la kuangazia Usalama wa Taifa katika Uwekezaji iliyofanyika kwa siku tano Jijini Dar es Salaam.
Alisema mafunzo hayo ni adhimu yenye lengo la kujenga Viongozi na wafanyabiashara katika uzalendo wenye kuzingatia usalama wa taifa letu katika sekta yenye kuingizia serikali mapato ya uwekezaji na kuipongeza NDC kwa mafunzo hayo na kazi kubwa ambayo wamekuwa wakiifanya katika kuwajenga viongozi.
“Mliopata mafunzo haya nataka mkawe chachu kwa wale amabao hawajayapata na kuwa tofauti katika Utendaji na Watendaji wengine ambao hawajapata mafunzo hayo kwani ni nafasi pekee amabayo sio kila kiongozi anaweza kuipata.” Alisema Waziri Solaga.
Awali Mkuu wa Chuo hicho Brigedia Jenerali Ibrahim Muhona alisema mchanganyiko wa kozi hiyo unatokana na ukweli kwamba sekta rasmi na sekta binafsi zinategemeana katika kukuza uchumi hasa katika kipindi hiki cha kuingia uchumi wa kati wa juu kama ilivyo dira ya mwaka 2025.
“Hali ya usalama na amani katika nchi yetu ni muhimu sana kwa jamii ya Watanzania na maendeleo kwa ujumla hivyo nyinyi ni wadau muhimu katika kuhakikisha adhma hiyo inatimizwa kikamilifu. Alisema Brigedia Jenerali Mhona