Kijana Mzalendo Bw.Frank Festo (Kulia)akiwa pamoja na rais wa Chuo cha Bahari (DMI) Bw.Salim Awali wakionesha stika yenye ujumbe “MIMI NASIMAMA NA MAMA SAMIA,WEWE JE”.
Kijana Mzalendo Bw.Frank Festo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam baada ya kukutana kwaajili ya uzinduzi wa stika yenye ujumbe “MIMI NASIMAMA NA MAMA SAMIA,WEWE JE”.
(Picha na Emmanuel Mbatilo)
*******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Ili kuweza kuunga mkono Juhudi za Rais Mhe.Samia Suluhu Hassani, Kijana Mzalendo Bw.Frank Festo amezindua stika yenye ujumbe “MIMI NASIMAMA NA MAMA SAMIA,WEWE JE”. Lengo kuhamasisha mshikamano, umoja, upendo, amani na furaha kama kipaumbele cha Rais Mhe.Samia Suluhu.
Akizungumza na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam, Bw.Festo amesema sote kwa pamoja tunapaswa kumuunga mkono ili kuweza kufanikisha kuiongoza Tanzania katika amani na upendo tulionayo toka zamani.
“Tusikae pembeni kwa kuchungulia na kumsikiliza eti huyu mama ataweza?.Kila mmoja awajibike kwa nafasi yake ipasavyo ndiyo njia pekee ya kumuunga mkono Mama yetu mpendwa”. Amesema Bw.Festo.
Aidha Bw.Festo amesema stika hiyo itasambazwa nchi nzima kupitia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, vyombo vya usafiri, kutembelea ofisi za Umma na Binafsi,Bunge, Shule,Vyuo na nyumba za ibada ikiwa lengo ni kuhakikisha ujumbe huo unamfikia kila mtanzania mahali popote alipo.
Pamoja na hayo Bw.Festo amesema kuwa pamoja na taifa letu kujaliwa rasilimali nyingi, rasilimali kubwa tuliokuwa nayo ni amani na hatuna mbadala wa amani.
Kwa upande wake rais wa Chuo cha Bahari (DMI) Bw.Salim Awali amewasihi viongozi ambao wamepewa dhamana serikalini kufanya kazi kwa bidii bila kumkatisha tamaa Rais kwa masirahi ya nchi yetu.
“Sisi kama vijana tunamuahidi Rais wetu tutaliendeleza taifa hili kwa umoja na kumshauri ni nini kifanyike ili tuweze kufika sehemu ambayo tunaitaka kwasababu kiongozi wetu Rais Mhe.Samia ni mtu ambaye anapokea ushauri na ni mtu ambaye msikivu”. Amesema Bw.Awali.