*************************
NA EMMANUEL MBATILO
Klabu ya Simba Sc imeambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Al Ahly katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi kwenye michuano ya CUF Champion League.
Licha ya Simba Sc kufungwa katika mchezo huo bado itakuwa inaongoza kundi hilo hivyo sasa inasubiri kupangwa kwa droo ya robo fainali kufahamu atacheza na nani kwenye hatua hiyo.
Bao la Al ahly liliwekwa kimyani na Mshambuliaji wao Mohamed Sherif dakika ya 32 kipindi cha kwanza.
Hata hivyo kwenye mchezo huo Simba Sc ilionekana kucheza kandanda safi la kumiliki mpira ingawa ilipoteza mchezo huo.