Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga,akizungumza wakati akifunga Mkutano wa 28 wa Baraza la 10 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliomalizika leo April 9,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo,akizungumza wakati wa Mkutano wa 28 wa Baraza la 10 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliomalizika leo April 9,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Ualimu ambaye pia ni Katibu wa Baraza Bw.Huruma Mageni,akielezea walivyojifunza wakati wa Mkutano wa 28 wa Baraza la 10 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliomalizika leo April 9,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa TUGHE Taifa Bw. Archie Mntambo,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wa Mkutano wa 28 wa Baraza la 10 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliomalizika leo April 9,2021 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Omary Kipanga, wakati akifunga Mkutano wa 28 wa Baraza la 10 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliomalizika leo April 9,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kipanga,amefunga Mkutano wa 28 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo huku akiwataka watumishi wake nchini kuzingatia maadili ya kazi ili kuweza kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.
Mhe.Kipanga amefunga Mkutano huo wa Baraza la 10 la wafanyakazi uliomalizika leo April 9,2021 jijini Dodoma.
Mhe.Kipanga amewataka watumishi hao kuzingatia yale yote waliyoelekezwa na Waziri wa wizara hiyo, Prof Joyce Ndalichako jana wakati akifungua baraza hilo ambapo alisisitiza nidhamu kazini na kuacha kutumia lugha za ubabe kwa wateja ambao ni wananchi.
Aidha ametoa wito kwa vyama vya wafanyakazi kama TUGHE na Chama cha Walimu Tanzania CWT kushirikiana na Menejimenti ya Wizarahiyo ili kuhakikisha wanasimamia ipasavyo nidhamu na kukuza ubunifu kwa wafanyakazi lengo likiwa ni kuifanya wizara izidi kufanya vizuri kama ambavyo ilisifiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
” Nawaomba watumishe wetu muendeleo na ushirikiano ili tuzidi kupongezwa kwa kufanya kazi vema ni lazima tushikamane tukiwa wamoja na wenye upendo, niombe kwa pamoja tuwe mabalozi wazuri wa kusimamia nidhamu na uwajibikaji kwenye vituo vyetu vya kazi”amesisitiza Mhe.Kipanga
Wizara yetu ndio uti wa mgongo wa Taifa letu, bila kukuza kiwango cha elimu na kuzalisha watalaamu wengi nchini ni vigumu kama Taifa kupata maendeleo, ni vema tukatoka na mkakati wa kuhakikisha tunazalisha vijana wasomi wenye tija kwa Taifa letu katika kuajiriwa na kujiajiri wenyewe,” Amesema Kipanga.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk Leonard Akwilapo amesema kuwa watayafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa kwao na Waziri Prof Ndalichako na kuwa watatekeleza yale yote yaliyokusudiwa na baraza hilo katika kukuza kiwango bora cha elimu nchini.
Nae Mwenyekiti wa TUGHE Taifa Bw.Archie Mntambo amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa bidii na ufanisi mkubwa ili kulinda sifa ya wizara hiyo ambayo imekuwepo kiasi cha kupokea sifa kutoka kwa Rais Samia.