………………………………………………………………………………….
Kufuatia maelekezo aliyotoa Mhe. Rais Mama Samia Suluhu Hassan yanayohusu tasnia ya habari nchini, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa (katikati kulia) amekutana na mmiliki wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Bw. Said Kubenea (katikati Kushoto).
Kubenea alifika ofisini kwa Waziri leo April 9, 2021 baada ya mapema wiki hii Mhe. Bashungwa kutoa fursa kwa wamiliki wa magazeti yaliyofungiwa kufika ofisini kwake kwa majadiliano zaidi.
Waziri Bashungwa ametoa wito kwa wadau wa tasnia ya habari kuunga mkono dhamira ya Mhe Rais Mama Samia kuona haki ya uhuru wa habari inaendana na wajibu na uzingatiaji sheria, kanuni na misingi ya taaluma ya habari.