Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiongoza wadau kutoka Kisima cha Mafanikio na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (WWF) upandaji miti katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Aprili 9, 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wadau kutoka Kisima cha Mafanikio na DShirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (WWF) wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Aprili 9, 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wa mazingira ambao pia ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya Ben Pol na Mwasiti Almasi na wadau kutoka Kisima cha Mafanikio na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (WWF) waliposhiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Aprili 9, 2021.
**********************************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo ameelekeza kuwa zoezi la upandaji miti liwe endelevu ili kusaidia kuhifadhi mazingira.
Jafo ametoa agizo hilo leo Aprili 9, 2021 wakati akiongoza zoezi la upandaji miti lililofanyika katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo Aprili 9, 2021 lililoshirikisha wadau mbalimbali.
Akizungumza na wadau hao kutoka Kisima cha Mafanikio na Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira (WWF) aliwataka kuendelea kuhamasisha wananchi kupanda miti.
“Tunataka zoezi la upandaji miti liwe endelevu wananchi chukulie zoezi hili kama la kawaida wasisubiri Siku ya Mazingira ndo wapande miti, katika nyumba zetu angalau kila moja iwe na miti mitatu au minne na kwa pamoja tutaweza kuifanya Dodoma na Tanzania kwa ujumla kuwa ya kijani,” alisisitiza.