Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu ripoti za mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2020.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu ripoti za mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2020 akiwa pamoja na wajumbe wa wa Kamati ya Hesabu za Serikali.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya LAAC,Mhe.Grace Tendega ,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo April 8,2021 jijini Dodoma wakati wa ripoti za CAG mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2020,Kushoto kwake ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Charles Kichere na kulia kwake ni Mjumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali Mhe.Deus Sangu
………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
RIPOTI ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imesema kuwa katika miradi ya maendeleo, wafanyakazi 2,408 kati ya 1,538 wa kigeni wanaojenga reli ya kisasa-SGR kipande cha kwanza na cha pili kutoka Dar es Salaam hawakuwa na vibali vya kazi.
Hayo yamesemwa leo April 8,2021 jijini Dodoma na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwasilisha ripoti hiyo kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 20, 2020, amesema kuwa hali hiyo ni kinyume naKifungu cha 9 (2) (a) cha Sheria za ajira za raia wa kigeni ya mwaka 2015.
“Mapitio yaripoti ya maendeleo ya kazi Novemba, 2020 yalibaini raia wakigeni 586 kati ya 924 walioajiriwa kwenye kipande cha kwanza ujenzi wa reli ya kisasa hawakuwa na vibali vya kufanyakazi.
“Hali hii pia ilibainika kwenye kipande cha ujenzi cha pili, raia wa kigeni 952 kati ya 1,484 hawakuwa na vibali vya kufanya kazi,” amesema .
Aidha amesema kuwa kutozingatiwa kwa vibali vya kazi kulisababisha kutolipwa ada ya vibali vya kazi inayofikia Dolaza Marekani 1,538,000 sawa na sh. 3,537,400,000 (kiwango cha ubadilishaji kilichotumika ni 2,300).
“Mahojiano zaidi na Maafisa wa TRC (Shirika la Reli Tanzania) yalionesha Idara ya Uhamiaji ilitoa idhini ya raia hao wa kigeni kutumia visa ya biashara kuendelea na kazi wakati maombi yao ya vibali vya kazi ya kishughulikiwa.
“Hata hivyo,ilielezwa wazi katika barua hiyo kwamba kutolewa kwa viza ya biashara hakikuwa kisingizio cha kutokuwa na vibali vyakufanya kazi kwaraia hao ambao waliajiriwa katika mradi wa SGR,” amesema Bw.Kichere
CAG pia amebainisha kuwepo raia wa kigeni 1,026 wanaofanya kazi katika mradi wa SGR (kwa vipande vyote viwili) wasiona vyeti vya sifa zao za masomo.
“Ripoti ya Maendeleo ya kazi Novemba, 2020 ilionesha kuwa vyeti vyao vilikuwa vikiendelea na michakato anuwai ya uthibitishaji.
“Hatahivyo, asilimia 83 kati yao bado walikuwa wakisubiri kwa sababu ilibainika waombaji hawakuwa na vyeti halisi vya masomo na walikuwa wakingojea kuvipokea kutoka Uturuki,” imefafanua taarifa hiyo.