Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma leo, ambapo ametangaza majina kumi ya madereva waliofungiwa kuendesha mabasi kutokana na ukiukaji wa sheria za usalama barabarani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji jijini Dodoma leo, ambapo ametangaza majina kumi ya madereva waliofungiwa kuendesha mabasi kutokana na ukiukaji wa sheria za usalama barabarani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
******************************
NA.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene, amewafungia leseni madereva 10 wa mabasi ya abiria yaendayo mikoani kwa muda wa miezi mitatu kwa kuvunja sheria ya usalama barabarani.
Hayo ameyasema leo April 1,2021 jijini Dodoma Mhe.Simbachawene amesema kuwa baadhi ya madereva wamenzisha tabia ya makusudi kukiuka sheria za barabarani na hivyo kuhatarisha maisha ya abiria wanaotumia vyombo hivyo na kupata ajali au kusafiri kwa mashaka.
Hatua hii imekuja kufuatia ajali ya basi la Machame Investment iliyoua watu nane na kujeruhi watu 19 likitokea Dodoma kuelekea mkoani Arusha ambapo kimsingi hali hiyo inachukuliwa kama uvunjifu wa sheria.
Mhe.Simbachawene ameliagiza jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabarani ,kuwachukulia hatua kwa kuwapeleka mahakamani madereva wote 10 ambao wamebainika kukiuka sheria barabarani kwa kuendesha kwa mwendo kasi.
Mhe. Simbachawene amewataja madereva hao wanaotakiwa kufungiwa leseni zao kuwa ni pamoja na Allan Msangi wa Kampuni ya Kapricon yenye namba T605DJR inayofanya safari za Dar –Moshi mwendo wa kl 125 kwa saa ,Husein Abdalah Dudu wa kampuni ya Kimotco Intertrade inayofanya safari Arusha kwenda Musoma (T520CXE)kwa mwendokasi wa Kl 25 kwa saa.
Amewataja wengine ni Seleman Shida Seleman wa Al-Saed (T313DSO)linalofanya safari za Dar-Kilombero huku likiwa na mwendo kasi wa Kl 103 kwa saa,Athman Shaban Mnzava wa Kampuni ya MB Coach (T391)yenye safari za Dar-Arusha likiwa na mwendokasi wa Kl 107 kwa saa,Juma Ally Simba wa Baraka Clasic (T340DPW) ya Dar-Masasi kwa mwendo wa Kl 107,Salum Mohamed Salum wa Kampuni ya mabasi ya Nice(T121DEA) yenye safari za Dar-Tunduru kwa mwendo wa Kl 110 kwa saa na Frank Alex Masawe wa basi la Machinga lenye safari za Dar-Mtwara (T694DRB)kwa Kl 95 kwa saa.
“Madereva wengine ni pamoja na Innocent Thomsoni wa Ester Luxury linalofanya safari za Moshi-Dar likiwa na Kl 107kwa saa lenye namba za usajiri T225DTB,Naseeb Nasor wa NBC Classic la Tabora –Kigoma (T565BED) na Maiko Mkindi wa Kilimanjaro Express linalofanya safar za Dar-Arusha (T675DHY) kwa mwendo wa Kl 100 kwa saa,”alisema Waziri huyo.
Aidha Simbachawene amewaagiza wamiliki wa mabasi hayo ambao madereva wao wamekiuka sheria ya usalama barabarani ,kuhakikisha wanachukua hatua stahiki kwa madereva wao ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha mara kwa mara umuhimu wa kufuata sheria barabarani.
“Natoa wito pia kwa madereva wote kuhakikisha wanafuata na kuheshimu sheria za usalama barabarani ,madereva wa mabasi ya abiria wanapaswa kuwa na sifa za maalum ili kupunguza ajali za barabarani,”amesema