Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya aliyesimama katikati akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Sustainable Agriculture Tanzania (SAT) Janet Maro aliyesimama kushoto na Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo Utafiti na Huduma za Ugani Wilhelm Mafuru wakikaa kimyaa kama ishara ya kumkumbuka Hayati Rais John Pombe Magufuli kabla ya kuanza kwa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya mafunzo kwa njia ya mtandao Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma leo tarehe 30 Machi, 2021.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akiwahutubia Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo waliohudhuria hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akisisitiza jambo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akiwahutubia Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo waliohudhuria hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Kilimo KATRIN Shedrack Kihombo Televisheni katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akimkabidhi ‘Projector’ Mkuu wa Chuo cha Kilimo HORTI – Tengeru Fahmia Suleima katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Mahinya Janet Lupenza ‘Camera’ katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya katikati akiwa na Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo pamoja na Wadau wengine mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya mafunzo kwa njia ya mtandao
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya akifurahia jambo pamoja na Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo pamoja na Wadau wengine
…………………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu Wizaa ya Kilimo Gerald Kusaya ametoa vifaa vya mafunzo kwa njia ya mtandao (E- Learning) kwa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo vya Serikali na Binafsi vyenye thamani ya shilingi milioni 242.
Hafla hiyo imefanyika leo Machi 30,2021 katika Ofisi za Wizara ya Kilimo zilizopo jijini Dodoma
Vifaa hivyo vya mafunzo kwa njia ya mtandao ni pamoja na Projector – 14; CPU – 14, Televisheni za LCD – 14, Camera – 28, Betri za seli kavu – 14, Inverter – 14, UPS – 84, Rooter za Mtandao – 13, Waya za HDMI – 57; Vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 242,066,959.30.
Katibu Mkuu Kusaya amekabidhi vifaa hivyo kwa Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo 29 ambapo Vyuo vya Serikali ni 14 na vya Binafsi ni 15 katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Kusaya amesema vifaa hivyo vya mafunzo kwa njia ya TEHAMA vimetolewa kwa Vyuo vya Mafunzo ya kilimo kwa sababu Vyuo hivyo ni kitovu cha kuzalisha Wataalam wa kilimo kwa lengo la kutoa maarifa na ujuzi kwa Wakulima ili wazalishe kwa tija na kujiongezea kipato.
Katibu Mkuu Kusaya ameongeza kuwa vifaa hivyo ni vya kisasa na vitachangia katika kurahisisha utoaji wa mafunzo kwa njia ya mtandao.
“Ili kufanikisha kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao, ni muhimu sana kuwa na vifaa vya kisasa na vyenye uwezo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa mtandao na vifaa vinavyowezesha mtandao huo kutumika.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kusaya.
Katibu Mkuu Kusaya aliendelea kusema kuwa “vifaa hivi vitaviwezesha Vyuo angalau kupiga hatua katika dhana ya TEHAMA ili kwamba pale ambapo baadhi ya vitabu havipatikani katika maktaba zetu, wanafunzi na wakufunzi waweze kuvipata kirahisi kwa njia ya mtandao. Aidha, ni matarajio yangu kuwa vifaa hivi vitatumika vizuri kwa manufaa ya wanufaika”.
Katibu Mkuu ameongeza kuwa Vyuo hivyo bado vinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na ukosefu wa vifaa vya kufundishia vinavyoendana na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo njia ya Mtandao (e-learning).
Wakati huo huo Katibu Kusaya amemshukuru Janet Maro Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sustainable Agriculture Tanzania (SAT) kupitia Mradi wa Kuwezesha Utekelezaji wa Mitaala katika Vyuo vya Mafunzo ya Kilimo vya Kati (Curriculum Implementation Support for Training Institutes-CISTI) ambapo wamekuwa wako bega kwa bega na Wizara katika kuhakikisha mafunzo yanaboreshwa.