RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa heshima za mwisho kwa mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa hafla ya kumuaga marehemu katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar leo 23/3/2021.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Zanzibar katika hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi katika hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt.Jon Pombe Magufuli katika uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
WANANCHI wa Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt.John Pombe Magufuli, aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Wananchi wa Zanzibar katika hafla ya kuuaga mwili wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania , hafla hiyo imefanyika katika Uwanja wa Amaan Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
******************************************
NA EMMANUEL MBATILO,ZANZIBAR
Rais Magufuli alikuwa mstari wa mbele kuimarisha maisha ya watanzania kwa misingi ya haki na usawa bila kujali dini, kabila, rangi wala jinsia hivyo kifo hiki kimetuachia simanzi kutokana na mapenzi makubwa tuliyonayo kwake kutoka na mambo mbalimbali ambayo marehemu aliyafanya kwa nchi yetu na bara la Afrika kwa ujumla.
Ameyasema hayo leo Rais wa Zanzibar Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Mwinyi wakati wa shughuli ya kumuaga Hayati Dkt.john Pombe Magufuli katika uwanja wa Aman Zanzibar.
Akizungumza katika tukio hilo Rais Dkt.Mwinyi amesema wataendelea kumkumbuka Rais John Pombe Magufuli kwa jinsi alivyojipambanua kupigania haki za wanyonge na kujidhatiti katika kudumisha Muungano wa Tanzania pamoja na kuyaenzi na kulinda Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
“Bado tuna huzuni kubwa kumpoteza Rais John Pombe Magufuli, Serikali zetu mbili kwa ushirikiano tumefanya juhudi kubwa kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kuonesha upendo kwa kuuaga mwili wa mpendwa wetu hapa Zanzibar ikiwa ni kuonesha na kutambua yale aliyoyatenda”. Amesema Rais Mhe.Dkt.Mwinyi.
Pamoja na hayo Rais Dkt.Mwinyi amesema watendelea kumpa ushirikiano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kufanikisha majukumu yake ya kuwatumikia watanzania,
“Binafsi namtambua fika kwamba ana uwezo mkubwa wa kuyafanikisha majukumu yake mapya kutokana na uzoefu wake mkubwa wa kisiasa na kiuongozi katika nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika”. Amesema Rais Mhe.Dkt.Mwinyi.