Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na wataalam wa menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa Utekelezaji wa Mipango ya menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe 19 Julai, 2019.
Mkurugenzi, Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akiongea na wataalam wa menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa Utekelezaji wa Mipango ya menejimenti ya maafa nchini, mjini Arusha, tarehe 19 Julai, 2019.
Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe (Wa pili kulia), kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kamisheni ya Menejimenti ya Maafa Zanzibar, Makame Khatib Makame, kushoto kwake ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Tanzania, Edward Anderson na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu (Utafiti na Mipango), Bashiru Taratibu, , wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, kwa taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti za maafa , mjini Arusha.
Baadhi ya wataalam wa masuala ya menejimenti ya maafa kutoka taasisi za serikali na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali yanayohusika katika menejimenti ya maafa wakijadiliana wakati wa zoezi la mezani la kupima uwezo wa utekelezaji wa Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa nchini, mjini Arusha Julai 16, 2019, zoezi hilo limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia.
***************
Benki ya Dunia, kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, imeendesha mafunzo ya siku tatu juu ya namna ya kufanya Tathmini ya mahitaji baada ya maafa kutokea na namna ya Kuandaa Mipango wa kurejesha hali baada ya maafa kutokea, kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na Idara za serikali pamoja na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali.
Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo, jijini Arusha leo tarhe 19, Julai, 2019, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amefafanua kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa na wataalam wa kutosha hapa nchini wa kufanya tathmini za Maafa kitaalam zenye kujikita katika athari za maafa katika nyanja za kijamii, kiuchumi na maendeleo.
“Mafunzo haya yatatusaidia kutuongoza serikali na wadau wa menejimenti ya maafa kuwa na mfumo wa pamoja utakao wezesha kuwa na mtazamo wa pamoja katika kuendesha shughuli ya Tathmini hususani kwa athari za kiuchumi kwa ngazi ya mtu binafsi, Taifa na Kimataifa, Uharibifu wa miundo mbinu na hapo tutaweza kuwa na mpango wa pamoja wa kurejesha hali ” amesema Matamwe.
Matamwe ameendelea kufafanua kuwa kutokana na wataalamu hawa kujengewa uwezo wa Kuandaa Mpango wa kurejesha hali, utaalamu huo utaisaidia nchi yetu Tanzania kuwa na Takwimu za urejeshaji hali ambazo tutapata uwezo wa kurejesha hali itakayo saidia nchi yetu kuwa inarejesha hali wakati.
Akiongea katika mafunzo hayo kwa niaba ya Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Mtaalamu wa Mawasiliano Benki ya Dunia Edward Anderson amefafanua kuwa Benki hiyo imeamua kuendesha mafunzo hayo ili nchi ya Tanzania kuwa na wataalam wenye uwezo wa kurejesha hali kwa wakati baada ya maafa kutokea.
“Tangu mwaka 2016 nilipofika hapa nchini nimeshuhudia athari za maafa yakitokea ikiwemo tetemeko la ardhi mkoani Kagera, na mafuriko katika jiji la Dar es salaam mwaka 2016, hivyo maafa yanahitaji mfumo sahihi na Mpango bora katika kurejesha hali, na ninafurahi kuona Benki ya Dunia tupo tayari katika kutekeleza hayo” Amesema Edward.
Aidha, washiriki wa mafunzo hayo kwa nyakati tofauti wamefafanua mafunzo hayo yamewajengea uwezo katika kufanya Tathmini baada ya maafa kutokea na uuandaaji wa Mpango wa kurejesha hali hususani katika maeneo ya kuanisha gharama za urejeshaji, mbinu za kuanisha vyanzo vya rasilimali fedha wakati wa urejeshaji hali, kuainisha hasara na athari zitokanazo na maafa .
Mafunzo hayo yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 16 hadi 19 Julai, 2019, liliwashirikisha wataalam wa usimamizi wa shughuli za maafa , kwa wataalamu wa menejimenti ya maafa kutoka wizara, mikoa, Taasisi na Idara za serikali pamoja na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali, limeratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Menejimenti ya Maafa, kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.