![](https://fullshangweblog.co.tz/wp-content/uploads/2021/03/Tuliapic.jpg)
AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI MRATIBU WA MATUKIO MWANTUM MGONJA ALISEMA WAMESHAMTUMIA BARUA KINACHOSUBIRIWA NI MAJIBU.
“TUNASUBIRIA MAJIBU ILA TUNAIMANI ATAKUBALI NA KUWA MGENI RASMI KATIKA PAMBANO LA NGUMI ZA KULIPWA KWA WANAWAKE” ALISEMA MWANTUM.
ALIONGEZA KUWA PAMBANO HILO NI LA KIHISTORIA KWANZA KWA KUKUTANISHA WANAWAKE MAARUFU WA NGUMI LAKINI PIA WANAWAKE KUCHEZA MKANDA MKUBWA KWA RAUNDI KUMI.
“WANAWAKE TUNAWEZA SASA KUDHIHIRISHA HILO PAMBANO LA KIHISTORIA LA MASUMBWI LINAKUJA NA LITAKUWA LA MFANO NA TUNATUMAINI MGENI RASMI ATATUKUBALIA OMBI LETU” ALISEMA MWANTUM.
MWANTUMU ALITOA WITO KWA WADAU MBALIMBALINKUJITOLEZA KUDHAMINI PAMBANO HILO KWANI ITAONGEZA MOYO NA KUPATA MASLAHI MAZURI YATAKAYOPUNGUZA CHANGAMOTO ZA MAISHA.
PIA ALISEMA ANAMATUMAINI KUWA LICHA YA FEDHA WADAU WATAJITOLEZA KUSAIDIA WAPATE BIMA ZAAFYA KWA KUANZIA MWAKA MMOJA ITAKUWA FURAHA KWETU WAANDAAJI.
ALIWATAJA MABONDIA WATAKAOWANIA MKANDA WA DUNIA SIKU HIYO KUWA NI HALIMA VUNJA BEI ATAKAYEPIGANA NA ZULFA MACHO KATIKA MCHEZO WA ROUNDI 10.
MABONDIA WENGINE NI FATUMA YAZIDU ATAKAYEPIGANA NA DOROTHEA MUHOZA, HAPPY DAUDI DHIDI YA LEILA YAZIDU NA LULU KAYAGE DHIDI YA JESCA MFINANGA.
WENGINE NI MWAMNE HAJI DHIDI YA SARAFINA JULIUS,AGNES KAYANGE DHIDI YA MWAJUMA PENGO,GRACE MWKAMELE DHIDI YA ASHA GOTA WAKATI SALMA KIHOMBWA DHIDI YA MARIAM MUNGI NA ZAWADI KUTAKA DHIDI YA MARTHA KIMARO.