Wito umetolewa kwa wazazi wote ambao hawajapeleka watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza shuleni ,kuwapeleka kwani wanavyowaweka ndani wanawanyima haki zao za msingi ya kupata elimu .
Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakati akipokea msaada wa mifuko 115 ya saruji ilioyotolewa na taasisi ya huduma ya new life Outreach iliopo wilayani humo mkoani Arusha ambapo alibainisha kuwa pamoja na shule kufunguliwa wapo baadhi ya wazazi ambao hawajawapeleka watoto shuleni.
Alisema kuwa wao hawataki kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba,mlango kwa mlango kuwatafuta watoto waliofaulu na hawajaenda darasani ili waende shuleni bali aliwaomba wazazi kuwapeleka watoto shuleni kwani kwani serikali inatoa elimu bure ,madarasa yamejengwa ,madawati yapo na kwasasa kutokana na misaada hii ilioletwa watakuwa na wigo mpana wa kujenga madarasa mengine.
“msaada huu wa mifuko 115 ni muendelezo wa kampeni tulioianzisha kama wilaya ya ujenzi wa madarasa ambayo sisi tulianzisha kwa lengo la kuhakikisha wanafunzi wote ambao wamefaulu wanapata nafasi za kusoma ,nataka kuwahakikishia wananchi wa wilaya ya Arumeru mifuko hii inaunganisha nguvu na jitiada ambavyo serikali inafanya ya kuhakikisha kila shule inakuwa na madarsa a nipo hapa kuwaambia kuwa kampeni yetu ya ujenzi wa madarasa imetupa matokeo chanya”alisema Muro .
Alisema kuwa katika wilaya ya Arumeru pamoja na kuongoza ufaulu wa kidato cha nne na kidato cha sita lakini kumekuwa na kampeni endelevu ya ujenzi wa madarasa na kwasasa wanafunzi wote ambao wameanza kidato cha kwanza idadi yote, ambayo wamepewa na tamisemi wanafunzi wote wamepata madarasa na wote wanaviti vya kukali hivyo anatumaini kuwa wazazi wataendelea kuwaunga mkono kwa kuwapeleka Watoto waliobaki majumbani shuleni.
Akikabidhi msaada huo mwinjilisti wa kimataifa ambaye pia ni mwenyekiti wa huduma ya New Life Outreach, Egon Falk alisema kuwa wameamua kutoa msaada huo wa mifuko ya saruji 115 kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Magufuli katika swala zima la utoaji wa elimu bure ,kwani anaelewa kuwa ukimuandaa mtoto vyema kwa kumpatia elimu ataweza kuwa kiongozi bora wa baadae .
“mimi napenda Tanzania pia napenda watu wa Tanzania hivyo niwaombe tu katika kila jambo wamtangulize Mungu katika kila jambo kwani yeye tu ndio anaweza kuwasaida hata katika swala hili la ugonjwa wa Covid 19 ameweza kusaidia nchi yetu ,nanimpongeze pia Rais kwa kuwa na Imani ya kutosha ya kumuamini Mungu hadi anaweza na ndio maana hakuruhusu wananchi wake waingie kizuizini kwa ajili ya ugonjwa huu hii inaonyesha ni kiasi gani ambavyo anamwamini Mungu kuwa ni muweza wa yote”alisema Egon
Aliwataka watanzani kundelea kuchukuwa taadhiri zinazotolewa huku wakimtanguliza Mungu Zaidi kwani yeye pekee ndio anaweza kuponya na kuondoa ugonjwa huu ,huku akiwataka waondoe hofu kwani Mungu amesikia maombi yao na ugonjwa huu autaendelea kuwauwa watanzania tena .
Kwa upande wake afisa uhusiano wa taasisi hiyo ambaye pia ni katibu hamasa wa wilaya ya Arumeru Nikolaus Sawa alisema kuwa taasisi yao imetoa mifuko ya saruji 115 yenye dhamani ya shilingi milioni mbili ,ambapo wao kama taasisi waliamua kusaidia katika sekta hii,ambapo pia aliwataka Wananchi wote ambao ni wadau wa elimu wajitokeze kusaidia katika swala zima la elimu ,kwani hakuna Tanzania nyine , nchi yetu ni moja hivyo tuisaidie ili iendelee kupanda kiuchumi .