Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa bara bara zinazounganisha Wilaya za Kongwa, Kiteto, Chemba na Kondoa ambazo tayari Wakandarasi wapo site kuzikarabati baada ya kutengewa fedha, barabara zinazotarajiwa kukamilika mwezi juni 2021.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mkoa wa Dodoma Mhandisi Salome Kabunda akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Mkuu wa Mkoa wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa bara bara zinazounganisha Wilaya za Kongwa, Kiteto, Chemba na Kondoa ambazo tayari Wakandarasi wapo site kuzikarabati baada ya kutengewa fedha, barabara zinazotarajiwa kukamilika mwezi juni 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akikagua daraja la Zoisa linalounganisha Wilaya za Kongwa na Kiteto wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa bara bara zinazounganisha Wilaya za Kongwa, Kiteto, Chemba na Kondoa ambazo tayari Wakandarasi wapo site kuzikarabati baada ya kutengewa fedha, barabara zinazotarajiwa kukamilika mwezi juni 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge akikagua bara bara inayounganisha Wilaya za Kiteto, Chemba na Kondoa wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa bara bara zinazounganisha Wilaya za Kongwa, Kiteto, Chemba na Kondoa ambazo tayari Wakandarasi wapo site kuzikarabati baada ya kutengewa fedha, barabara zinazotarajiwa kukamilika mwezi juni 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Dkt Sulemani Serela akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa kukagua ukarabati wa bara bara zinazounganisha Wilaya za Kongwa, Kiteto, Chemba na Kondoa ambazo tayari Wakandarasi wapo site kuzikarabati baada ya kutengewa fedha, barabara zinazotarajiwa kukamilika mwezi juni 2021.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mkoani Dodoma Simon Chacha akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa kukagua ukarabati wa bara bara zinazounganisha Wilaya za Kongwa, Kiteto, Chemba na Kondoa ambazo tayari Wakandarasi wapo site kuzikarabati baada ya kutengewa fedha, barabara zinazotarajiwa kukamilika mwezi juni 2021.
………………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Kongwa
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amewaagiza wakandarasi wanaokarabati barabara zinazounganisha Wilaya za Kongwa, Kiteto, Chemba na Kondoa kuzingatia ubora na viwango sambamba na kuzikamilisha kwa wakati.
Wakandarasi hao ni anayekarabati barabara ya Kongwa hadi Dosi dosi mpakani na Wilaya ya Kiteto kampuni ya Musons Engeneers na Technics Construction Group Limited anayekarabati bara bara ya Mrijo hadi Kolo Kondoa na Afritrast Group Limited inayokarabati bara bara ya Bicha hadi Mondo Wilaya ya Chemba.
Dkt Mahenge ametoa maagizo hayo baada ya kukagua barabara hizo na kubainisha kuwa bara bara hizo ni muhimu katika usafirishaji wa mazao hivyo ni lazima zikarabatiwe kwa ubora na viwango vinavyotakiwa.
Amesema katika ziara hiyo imelenga kukagua utayari wa miondombinu hiyo baada ya mvua kunyosha kisha kuanza kukarabatiwa kwa kuwa bara bara ni muhimu hasa kwa kuwa Wilaya hizo ni wakulima.
“Nimekuja kuangalia bara bara hizi tunajua mvua zimenyesha na njia zote tulizopita mazao yamekubali baada ya kipindi cha mvua kuisha mazao yatatakiwa kusafirishwa nimekuja kuona je bara bara zinautayari” amesema Dkt Mahenge.
Ameongeza kuwa ” Tumeona bara bara hizi zimeanza kukarabatiwa hivi karibuni tunakumbuka kwenye kikao cha bara bara tuliambiwa wakandarasi wapo site lakini fedha hamna lakini sasa fedha imetoka nimekuja kuona je kazi zinaendelea?” amesema.
Amesema Serikali ina mpango wa kujenga barabara ya lami kutoka Handeni Tanga, Mrijo, Chemba hadi Singida ambapo zitaweza kufungua shughuli za kiuchumi katika Mikoa hiyo.
Amewataka wananchi kuacha kufanya shughuli zozote kando ya bara bara hizo hasa kilimo sambamba na kupitisha mifugo ili barabara ziweze kudumu kwa mda mrefu na wananchi wakaepukana na madhara yanayotokana na miondombinu ya barabara kuwa mibovu.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa barabara nchini TANROADS Mkoa wa Dodoma Mhandisi Salome Kabunda amesema bara bara zote tayari zinawakandarasi wanaendelea na ukarabati wa bara bara hizo.
Amesema bara bara ya njia panda ya Hogolo Kongwa hadi Dosi dosi mpakani na Wilaya ya Kiteto Manyara inayokarabatiwa kwa shilingi milioni mia tano themanini (580) ambayo pia ilijumuisha ukarabati wa daraja la Zoisa ambalo liliharibiwa na mvua na kulikarabati kwa mda kusubiri ujenzi wa daraja jipya.
Pia amesema kipande cha bara bara ya Kibaya Wilaya ya Kiteto Manyara hadi Mrijo Wilaya ya Chemba nayo tayari ina mkandarasi ambaye bado hajaanza kuikarabati na itaanza kukarabatiwa hivi karibuni.
Amebainisha kuwa barabara kati ya Mrijo hadi Kolo Wilaya ya Kondoa nayo tayari imeenza kukarabatiwa na mkandarasi Technics Construction Group Limited inayokarabatiwa kwa shilingi milioni mia nane (800) ikijumuisha uchongaji wa barabara na ujazaji wa kifusi kwenye maeneo korofi.
Pia kipande cha Bicha hadi Mondo Wilaya ya Chemba ambayo nayo tayari mkandarasi yupo site ambapo bara bara zote zinatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka 2021.