**************************************************
11/03/2021 DAR ES SALAAM
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika EAPCCO ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifuatilia mkutano wa Wakurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Shirikisho hilo, mkutano ambao umefanyika kwa njia ya mtandao Video Conference na kufunguliwa na Mwenyekiti wa Shirikisho hilo ambapo Wakurugenzi hao watatumia fursa ya mazungumzo kwa kujadiliana masuala ya ugaidi, ukatili wa kijinsia pamoja na masuala ya haki za binadamu. Picha na Jeshi la Polisi