MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu katikati akizungumza wakati akifungua kikao cha Jukwaa la Wadau wa Machungwa wilayani humo kushoto ni Afisa Kilimo wa wilaya ya Muheza Hayange Mbwambo na kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo
Afisa Kilimo wa wilaya ya Muheza Hayange Mbwambo akizungumza wakati wa Jukwaa hilo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu
Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Benard Mhagama akizungumza katika Jukwaa hilo
MBUNGE wa Viti Maalumu (Chadema) Mkoa wa Tanga Yosepher Komba akizungumza katika Jukwaa hilo
Mtaalamu wa Kilimo kutoka Chuo cha Kilimo Mlingano wilayani Muheza akisisitiza jambo kwenye Jukwaa hilo
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakifuatilia Jukwaa hilo
Sehemu ya washiriki wa Jukwaa la Machungwa wakifuatilia kikao
Sehemu ya washiriki wa Jukwaa la Machungwa wakifuatilia kikao hicho
Sehemu ya wadau kwenye Jukwaa hilo
Sehemu ya wadau wa kikao hicho
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu amesema anaumia sana anapoona zao la machungwa ambalo linalimwa kwa wingi wilayani humo kutokupata thamani kama yalivyokuwa mazao mengine hapa nchini.
Lakini pia amesema anapokaa na kuona zao la chungwa linaharibika kwa kutupwa onyoovyo jambo hilo limekuwa likiwakera na kuwapa wakati mgumu kutokana na kuona linashuhwa thamani yake iliyonayo
Balozi Adadi aliyasema hayo juzi wakati akizungumza katika Jukwaa la Wadau wa Machungwa lililofanyika wilayani humo na kushirikisha wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kifedha,wasafirishaji,wakulima ,vyama vya ushirika,wafanyabiashara ,walaji na wasindikaji.
Alisema kwamba kwani zao hilo ambalo linalimwa wilayani humo na tamu nchi nzima linapatikana huko lakini bado limekuwa halipewi thamani ambayo inashahili jambo ambalo limekuwa likimnyima raha kila wakati
“Mimi ni mdau wa zao machungwa na ninalima eka nyingi lakini ninapata uchungu ninapoona Tunda ,zao la hili ambalo linalimwa Jimboni kwangu Muheza na Tamu nchi nzima kuona halipati thamani ile ambavyo inastahili”Alisema Mbunge huyo.
Aidha pia alisema tunda hilo limekuwa halina thamani kutokana na kwamba wakulima wake tunauza kwa bei ya kutupa ndogo hivyo ninaamini jukwaa hili ni zuri kwa sababu hiyo changamoto kama hizo tutaona namna ya kuzipatia ufumbuzi kuweza kuondokana na hilo tatizo
Mbunge huyo alisema kwamba changamoto zinaanzia kwenye mbegu yenyewe ,ulimaji,utunzaji,uvunaji mpaka kwenye kuvuna,kuuza na soko lenyewe huo msururu wote una vikwazo vipo katikati na ndio maana kwenye jukwaa hilo wanatakiwa kukaa mara kwa mara ili kuweza kujua namna ya kukabiliana nazo.
Hata hivyo alisema kwamba wanapokaa na kuona zao la chungwa linaharibika linatupwa ovyoovyo inamuuma sana huku akieleza namna alivyopambana kuwashawishi wawekezaji na kuwafikisha wilayani humo .
“Niliwashai kuleta wawekezaji na mara ya kwisho walikuja wachina na wote wanasema matunda ya muheza ni matamu sana mazuri lakini ni machache kwa hiyo sio matunda ya kuweza kuweka kiwanda lakini ukipita barabarani machungwa yamesambaa lakini unaambiwa hawatoshi kuweka kiwanda wawekezaji wawili wamekiwsha kufika lakini naambiwa hivyo hii inaniumiza sana “Alisema
Awali akizungumza katika Jukwaa hilo Afisa Kilimo wa wilaya ya Muheza Hayange Mbwambo alisema wameamua kuitisha Jukwaa hilo ili kujadili kwa pamoja na wadau kwenye wilaya na nje ya wilaya hiyo changamoto za uzalishaji wa zao la machungwa na usindikaji kwa sababu wamegundua wilaya muheza ina uwezo wa kuzalisha kwa kiwango kikubwa zao hilo na kuwaletea wakulima kipato kikubwa kwa kukuza uchumi wao na halmashauri kwa ujumla.
Alisema kwamba muda mrefu wamekuwa wakizalisha zao la machungwa lakini changamoto nyingi ni magonjwa wakiwemo wadudu pamoja na tatizo la wafanyabishara wanaokuja kuwarubini wakulima kwa kuwapa fedha kabla ya machungwa kukomaa.
Alisema hali hiyo inapelekea kulazimisha kuivisha machungwa kwa moto na kufanya ubora wa machungwa kwenye soko kuwa mdogo lakini pia kufanya walaji wa wa nje ya wilaya kuona machungwa sio bora na hivyo mwisho ya siku inawezekana zao hilo likashuka kupata wanunuzi kutokana na kwa sababu ya ubora hafifu unaotokana na kulazimisha kuivisha machungwa kwa moto.
Mwisho.