Mgeni Rasmi Dkt. Phillis Nyimbi Mkuu wa Wilaya ya Nyamagamana akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria Kanda ya Mwanza Dkt. Ancyfrida Prosper Tibilengwa
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Jaji ya Mahakama Kuu ya Tanzania na Pia Mkuu wa Chuo Dr. Paul F. Kihwelo (kushoto) na Katibu wa Baraza Ndugu Farid Sechonge wakiendesha kikao kilichofanyika Machi 8, 2021 katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria jijini Mwanza
Wajumbe wa kikao cha baraza wwakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
****************************************
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagama Dkt. Phillis Nyimbi amelipongeza Baraza la Wafanyakazi la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa kutekeleza na kuzingatia mkataba wa baraza.
Akifungua kikao cha baraza Dkt. Nyimbi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mhe. George Mongela alisema madhumuni ya kufanya kikao Mkoani Mwanza ni kwa ajili jinsi gani wajumbe wa baraza la wafanyakazi mtashauri Baraza la Uongozi la Chuo jinsi ya kuviendeleza viwanja ambavyo vipo Mwanza na Simiyu.
Dkt Nyimbi kwenye hotuba hiyo alisisitiza kwa baraza hilo kuwa, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inahidi kuwa itatoa ushirikiano wa kutosha kwa Chuo wakati kinapoelekea kwenye kuwekeza katika kanda hii ya ziwa kwa kuzingatia Chuo kina maeneo katika Mkoa wa Mwanza na Simiyu.
Aidha Dkt. Nyimbi aliendelea kwa kusema, kufungua matawi ya Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto katika mikoa ya Mwanza na Simiyu itasaidia kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Aidha, Dkt. Nyimbi aliogeza kwa kutambua Chuo kinavyotekeleza kwa kiwango kikubwa Mpango Mkakati wa Chuo wa Miaka mitano pamoja na ule wa Mahakama katika eneo la Mafunzo. Pamoja na nyongeza hiyo Dkt Nyimbi alifarijika zaidi na Elimu bora inayotolewa na IJA kwa ngazi za Stashahada na Astashahada ili kuboresha sekta ya sheria na utoaji haki nchini na kufanya wananchi wengi kuongeza Imani na Chuo hiki kwa huduma zinazotolewa.
Aliwahimisha wajumbe wa baraza kuwa na kauli moja badala ya kila mmoja kuwa na uelekeo wakwe mwenye kwani taaisisi huendeshwa na watu na kama watu hao hawatakuwa na kauli moja inaweze kuharibu uhusiano wa ndani na baadaye kuharibu taswira ya Taasisi na kasha kuleta mahusiano mabaya na wadau na hii inaweze kuepelekea kuzorota kwa malengo ya Chuo.
Dkt. Nyimbi, hakusita kuwakumbusha wajumbe wa baraza kufanya kazi kwa kufuata miongozo na taratibu mbalimbali za kiutumishi ili kukiwezesha Chuo kusonga mbele. Aidha, alisema, ni muhimu kwa kila mjumbe wa baraza kuwa huru kuelezea malalamiko au kero kisheria kwa uongozi husika na namna inavyokubalika.
“Si vyema kuzungumza mambo yanaykuguza husko pembeni lakini inapofika mahali sahihi kama vile kwenye vikao kutofanya hivyo”
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo, Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi alifafanua zaidi kwa kusema baraza hili la wafanyakazi limefanyika Mwanza ili viongozi hawa wa baraza kuja kuona viwanja hivi na kuona jinsi gani ya kuviendeleza.