*****************************************
Na Woinde Shizza, ARUSHA
WATANZANIA wanapaswa kumshukuru Mungu katika janga la corona na kumuombea Rais Magufuli kwa kuwaondolea hofu kwa kuwa awali hofu ilikuwa inawaua kuliko corona.
Hayo yamebainishwa na Mwalimu Ezekiel Mollel alipokuwa akiongea katika ibada kanisa la kiinjili na Kilutheri nchini (KKKT) usharika wa Enaboishu wakati wa ibada ya shukrani ya familia ya Elphace Mollel iliyopo mtaa wa Oloigero.
Alisema kuwa watanzania wengi walikuwa wanakufa kutokana na hofu Ila baada ya Rais Magufuli kusimamia na kuwaambia wasiuogope na waondowe hofu hali imebadilika ,pia alimpongeza Rais Magufuli kwakuwa na msimamo wa kuzuia chanjo zisiingizwe nchini.
Alisema kuwa msimamo wa Rais wa Tanzania,Dkt John Magufuli kuhusu kutoruhusu uingizaji wa chanjo za corona hapa nchini ni wa kishujaa kwa kuwa watanzania hawawezi kutumika kama majaribio.
Pia amewashauri baadhi ya viongozi wa dini nchini kutoyumba kiimani kwa kuwa baadhi yao wamegawanyika na kukosa msimamo kutokana na ugonjwa wa corona,na kufafanua kuwa kitu ambacho viongozi wa dini wanatakiwa kufanya ni kukemea ugonjwa huu uondoke na sio kuanza kubeba majukumu ambayo sio yakwao.
Alisema kwamba Rais Magufuli hajapinga ujio wa chanjo ya corona lakini alichopinga ni chanjo hizo kutumika kwa watanzania kama majaribio.
Alibainisha kwamba anaamini Rais Magufuli ,pamoja na viongozi wengine wa serikali atawavusha watanzania salama katika janga la Corona na anathamini watu wake na hivyo msimamo wake wa kuzipinga chanjo hizo za majaribio unapaswa kuungwa mkono.
Hatahivyo,aliwashauri baadhi ya viongozi wa dini kuwa na msimamo katika imani kwa kuwa wao wamepewa jukumu la kuwachunga kondoo na sio kuwatia hofu.
Alisema nia ya kutoa shukrani katika ibada hiyo kwa niaba ya familia Dr.Ezekiel Mollel alisema kwamba anamshukuru Mungu kumponya mama yake mzazi aliyelazwa mahututi katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) akipumulia mashine pamoja na baba yake ambaye aligogwa na gari na kupona nandio maana ameamua kutoa shukrani kumshukuru Mungu
Awali Mchungaji aliyeongoza ibada hiyo,Samwel Laiser alisema kwamba pamoja na serikali kupitia wizara ya afya kutoa mwongozo katika kupambana na ugonjwa wa Corona lakini watanzania wanapaswa kumtegemea Mungu kwanza.
Alisema kwamba watanzania wanapaswa kuondokana na hofu katika kipindi hiki kwa kuwa ugonjwa wa corona ni janga litakalopita na kuwasihi wasimame imara muda huu kumtegemea Mungu katika maombi,sala na shukrani.
“Neno na Mungu ndilo linalotia nguvu endeleeni kumtumikia Mungu sote tuondoe hofu na mashaka pamoja na wizara ya afya kutoa maelekezo lakini maombi yawe nambari moja “alisema Laiser
Akitoa shukrani katika ibada hiyo kwa niaba ya familia Dr.Ezekiel Mollel alisema kwamba anamshukuru Mungu kumponya mama yake mzazi aliyelazwa mahututi katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) akipumulia mashine na ameamua kutoa shukrani kumshukuru Mungu.