**********************************
Na Woinde Shizza , ARUSHA
IMEBAINIKA kuwa sababu kubwa inayofanya wanawake washindwe kupiga hatua ni kuwa tegemezi ,pamoja na kutojiamini.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti wa Chama Cha kuweka na kukopa Arusha women in business saccos Aichi Temu wakati akiongea katika sherehe za kuazimisha siku ya mwanamke duniani,zilizoandaliwa na Chama hichi.
Alisema kuwa wanawake wengi wamekuwa wanashidwa kufanya Maendeleo kutokana na kuwa tegemezi kwa wanaume zao jambo ambalo limepitwa na wakati ,kwani kwa Sasa kila mwanamke anatakiwa ajitume na afanye kazi.
Alisema kuwa Chama chao Cha kuweka na kukopa kilianza mwaka 2018 na wanachama wachache lakini hadi Sasa wanawanawake zaidi ya 800 na wameshatoa mikopo ya zaidi ya Shilingi bilioni 18 kwa wanachama wao.
Aliwataka wanawake kupigania ndoto zao kwa nguvu zote Ili waweze kufikia malengo yao yao ya kujiletea Maendeleo.
Kwa upande wake mwanamke mfanyabiashara kutoka soko kuu lililopo mkoani hapa ,Mwantumu Shabani alipokuwa akiongea katika sherehe za maathimisho ya siku ya wanawake duniani ziliofanywa na kikundi Cha kuweka na kukopa Cha Arusha women in business saccos alisema ni vyema wanawake wakainuka na kuacha kuogopa kutekeleza ndoto zake.
Alisema wanawake wengi wamekuwa waoga wa kutekeleza malengo yao wengine wakiwa wanakwamishwa kutimiza na wanaume zao kitu ,kitu ambacho wanatakiwa kukikataana kusimamia walichonacho wapambanie walichonacho.
” Nilipoanza biashara nilikatishwa tamaa,nilitaka kuachwa muda mungine nilipigiwa na mume wangu lakini sikukata tamaa nilipambania nilichonacho ,sikufa Moyo na Sasa nimefanikiwa nimeweza kujenga nyumba nzuri,ninabiashara kubwa na mume wangu amekuwa na adabu maana ninaela hivyo tusikatishwe tamaa ya kutimiza malengo yetu”alisema Mwamtumu.
Akifungua sherehe hizo Afisa ushirika mkoa wa Arusha Peter Laswai alisema aliwataka kinamama kuendelea kuchukuwa tahadhari ya ugonjwa wa Covid 19 huku walifanya kazi kwa bidii Ili waweze kufikia malengo yao yakujiingizia kipato pamoja na kuingizia serikali yetu mapato.
Aliwapongeza Arusha women in business saccos kwa kuanzisha taasisi yao hii ya kuweka na kukopa na kusema kuwa ,mkoa wa Arusha unajumla ya vyama vya kuweka na kukopa 186 na Kati ya hizo vyama zaidi ya 15 ni wanawake tu.
Aliwataka kuendelea kushikamana Ili waweze kufikia malengo yao na waendelee kujipanga kuwa na miradi mikubwa zaidi ,wasiweze kukataa tamaa kabisa.