Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi,akizungumza wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi,akieleza jambo wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Binilith Mahenge,akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa uzuiaji rushwa wa TAKUKURU Bi.Sabina Seja,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi,(hayupo pichani) wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Kwaya ya TAKUKURU itoa burudani wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo,akimkabidhi muongozo wa TAKUKURU Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi,mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu uliofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu iliyofanyika leo March 2,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi,ameitaka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) kuhakikisha inaongeza kasi katika kukabiliana na kesi za ubakaji zinazopelekea mimba za utotoni.
Mhe.Ndejembi ameyasema hayo leo March 2,2021 jijini Dodoma wakati akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa viongozi wa TAKUKURU uliowakutanisha wakurugenzi,wakuu wa vitendo na watendaji wakuu.
Mhe.Ndejembi amesema kuwa pamoja na TAKUKURU kushughulikia kesi nyingi na kuwasaidia wanannchi waliodhulumiwa,bado suala la kesi zinazohusu mimba za utotoni linawatesa wanafunzi wengi hali inayowanyima kuendelea na haki ya masomo yao.
“Nategemea na hili mtalimaliza na hatimaye watoto wetu wataishi kwa amani bila kudhihakiwa kwenye jamii,naamini hasa ukizingatia mimi mwenyewe ni mnufaika wa TAKUKURU,bila ninyi kusimamia haki hata leo hii nisingesimama hapa,”amesema Mhe.Ndejembi.
Ndejembi amesema kuwa ikiwa mapambano ya rushwa ya ngono yatafanikiwa itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ongezeko la kesi za mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikimalizwa kimya kimya .
Awali Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo ameeleza kuwa wao kama watendaji wenye dhamana ya kuisaidia jamii kuondokana na vitendo vya rushwa watahakikisha wanatumia muda wao wote kupambana na waovu wanaokandamiza watu kwa rushwa ya ngono.
Brigedia Jenerali Mbungo amesema kuwa jamii inahitaji kuishi katika usawa hivyo Taasisi hiyo kwa kuzingatia Utumishi na Utunzaji wa siri watashirikiana beka kwa bega na jamii kuhakikisha uovu wote unaotokana na rushwa unadhibitiwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uzuiaji rushwa wa TAKUKURU Bi.Sabina Seja,amesema kuwa TAKUKURU kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo itaendelea kusimamia kwa dhati kesi za rushwa ya ngono na kuwapa haki wahanga ambao mara nyingi ni wanafunzi wa vyuo vikuu na mashuleni.
“Tutapambana na kusimamia haki bila upendeleo,mpaka pale hali itakapokua sawa,furaha yetu ni kuona jamii ikishi kwa amani bila vitendo vya rushwa kwa kuwa tunaamini rushwa ni adui wa haki”amesema Bi.Seja