Mkuu wa Iringa Alli Hapi akitoa akiwahutubia wakazi wa Miyomboni mjini Iringa wakati wa ziara yake ya kuhamasisha ufunguzi wa stendi mpya ya mkoa eneo la Igumbilo nje kidogo na mji wa Iringa iliyoanza kutumika jana

Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas (kulia) akimkabidhi fedha kiasi cha shilingi 500,000 kijana Maniani Mwakajenge ambae ni mjasiriamali aliyevunjwa mguu wake na polisi baada ya kijana huyo kulalamika katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa mkoa wa Iringa Alli Hapi juu ya polisi kushindwa kumlipa gharama za matibabu kiasi cha Shilingi milioni 1 pamoja na Asas kumsaidia pia mkuu wa mkoa alimchangia Tsh 500,000 kijana huyo

(Picha na Francis Godwin)

……………………..

NA  FRANCIS GODWIN, IRINGA

Mkoa  wa  Iringa Alli  Hapi ameliagiza  jeshi la polisi   kuwakata   mshahara  kiasi cha shilingi milioni 1 askari  wake 10 waliohusika kumvunja mguu  kijana Maiman Mwakajenge akiwa katika shughuli  zake  za ujasirimali   .

Kuwa  fedha  hizo  watakazokatwa  apewe  kijana  huyo aliyevunjwa  mguu kama sehemu ya kulipia gharama  zake  za matibabu   alizotumia baada ya  kuvunjwa mguu na askari hao .

Mkuu  huyo  wa  mkoa  alitoa agizo   hilo kwa kamanda  wa  polisi  mkoa wa Iringa  Juma Bwire  jana jana katika  eneo la  stendi  kuu ya  mkoa baada ya   kijana  huyo  Mwakajengela kulalamika  kwenye  mkutano wa mkoa huyo wa  mkoa  kuhusu  kutotendewa haki na jeshi la polisi baada ya  kuvunjwa mguu.

Kijana  huyo  alimweleza  mkuu  wa mkoa  kuwa  Februari 2  mwaka  huu  akiwa katika  shughuli zake za biashara  eneo la Samora  mjini Iringa alikutana na askari  polisi  waliokuwa doria  ambao  walimchukua na  kumpakia katika gari  la  polisi na  kuanza  kumshambulia kwa  kipigo na  kumvunja mguu wake  wa kushoto .

“ Askari  hao  walichukua uamuzi wa kunipiga hadi  kunivunja mguu  wakidai  kuwa  nimewatukana na baada ya kunivunja  mguu  nilifanyiwa  upasuaji  Hospitali ya  Rufaa ya  mkoa wa Iringa kwa gharama  zangu   kabla  ya   uongozi wa chama cha machinga  mkoa wa  Iringa kuingilia kati na  kukaa na jeshi la  polisi ambao  waliahidi  kuwa  watakuwa  akitoa  fedha  ya  chakula  na matibabu kwa  ajili yangu na familia  ila hadi  leo  hawafanyi  hivi na nawadai kiasi cha shilingi milioni 1  hadi  sasa  naomba  mheshimiwa mkuu  wa mkoa nisaidie  maana hadi hivi  sasa ninatembea na chuma mguuni “  alisema  kijana  huyo.

Kwa  upande  wake  Hapi  alimtaka  kamanda  wa  polisi mkoa  wa Iringa kwa  kuwa  anataarifa  ya  kuwepo kwa  tukio  hilo  lililofanywa na askari wake  kuwafuata   askari  wote  waliohusika ambao hata   hivyo wanafahamika   na  kuwakata  fedha  zao  za mshahara  ili  kumlipa  kijana  huyo  fedha  yake anayowadai ya gharama  za matibabu na chakula  kwa muda  wote ambao alikuwa Hospitali  kiasi  hicho  cha Tsh milioni 1 anayowadai.

‘’ Ninakuagiza RPC Bwire  fyeka misharaha  yao askari  sio  una posho  zao  za  mishahara   Nikishuka kama mwewe  nikawadokoa  itakuwa balaha  sawa   bwana utapewa  shilingi milioni 1 na mimi  kama mkuu  wako wa mkoa nitakuchangia  shilingi 500,000 na  MNEC  Salim Asas  nae namsemea  atakuchangia  shilingi 500,000”  alisema  mkuu  huyo wa mkoa huku akimkabidhi fedha  taslim kutoka kwake na MNEC  Iringa kiasi cha shilingi  milioni 1

Hata  hivyo  kamanda  wa  polisi  mkoa wa Iringa Juma Bwire  alithibitisha  kuwepo  kwa  tukio  hilo na kuwa atalifanyia kazi kwa  wakati .

Katika  hatua  nyingine  mkuu  huyo wa  mkoa ametangaza  kuvifuta  viwanja  vyote  vilivyopo mbele ya  stendi  kuu ya mkoa  wa  Iringa  iliyojengwa  eneo la Igumbilo viwanja  ambavyo  walijimilikisha  watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na baadhi ya madiwani  kuwa  viwanja  hivyo  vitatumika kwa  ajili ya wananchi  kujenga  maduka ya  biashara  kuzunguka  stendi hiyo .

“   Haiwezekani  stendi  kubwa kama  hii iliyojengwa na  serikali kwa  shilingi  bilioni 3   kujengwa  bila maduka  ya  biashara  ama kutenga maeneo ya  wafanyabiashara  kufanyia  shughuli  zao  ila  nimebaini  kuwa viwanja  vyote  vya  mbele  wamejigawia wao ili  kuja kunufaika  wao na stendi  hii  sasa sitaangalia kiwanja  kinamilikiwa na naibu meya  ama Meya  , diwani ama  mtumishi  wa Manispaa kuanzia  sasa  nimevifuta  vyote  na sitaki suala  hili  kujadiliwa  kwenye baraza la madiwani nataka  wananchi  wote  wapate maeneo ya  biashara  sio  vkiongozi “  alisema Hapi .