****************************************
Timu ya KMC kesho itakuwa katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Kurugenzi kutoka mkoani Simiyu mchezo utakaopigwa saa 16.00 jioni.
KMC FC inashuka Dimbani ikiwa imetoka kuifunga Timu ya Kagera Sugar magoli matatu kwa sifuri mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara na kwamba imejipanga kuhakikisha inaendeleza wimbi la ushindi katika mchezo huo.
Aidha katika mchezo huo, KMC inahitaji kupata ushindi kwa mara nyingine ambapo katika droo ya tatu ilishinda dhidi ya Lipuli magoli mawili kwa sifuri na kwamba imejipanga kuhakikisha inafanya vizuri katika mchezo huo wakesho wanapata matokeo mazuri ilikuendelea kujiimarisha kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kombe hilo.
“Michuano hii ambayo tunashiriki ni sehemu ya malengo yetu ya kuhakikisha kwamba tunakwenda kuchukua kombe hilo kwasababu uwezo tunao, nia tunayo, na kikubwa katika mchezo wakesho tunaingia tukifahamu katika tunacheza na Timu ambayo inahitaji kupata ushindi hivyo tumejipanga vizuri.
Hata hivyo katika mchezo wa kesho pia utatumika kujiweka vizuri katika kuendelea kufanya vizuri kwa michezo ya ligi kuu ambapo KMC FC itakutana na Polis Tanzania Machi Nne katika uwanja wa Sheih Amri Abeid Jijini Arusha.