Mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi akiongea na waandishi wa habari juu ya bonanza la Arusha Cup.
*******************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Waziri wa habari michezo utamaduni na sanaa Innocent Bashungwa anatarajiwa kufunga bonanza la Arusha cup huku watani wa jadi Simba na yanga wakisakata kabumbu katika bonanza hilo.
Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya bonanza hilo tangu lilipoanza januari 31,2021 na fainali kufanyika februari 27,2021 ambapo alisema kuwa katika michezo 24 iliyochezwa katika uwanja huo kila michezo umeingiza timu mbili fainali na watakao ibuka kidedea watakabidhiwa zawadu mbalimbali.
Alisema waziri Bashungwa ameshathibitisha uwepo wake na siku ya fainali wataanza na Mazoezi ya Arusha Jogging club na baada ya hapo michezo mbalimbali itaendelea na baadae mtanange kati ya Simba na Yanga hivyo wananchi wahudhurie kwa wingi kwani michezo ni afya.
Aidha alisema kuwa serikali kupitia fainali za bonanza la super cup na kwa kushirikishirikiana na wadau mbalimbali wataanzisha benki ya damu mkoani Arusha pamoja ba kuendesha zoeozi la uchangiaji wa damu.
“Benki ya damu inayotegemewa na mkoa wa Arusha ni benki ya kanda nzima ambayo ipo Mkoani kilimanjaro lakini kupitia bonanza hili kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tuataanzisha benki ya damu hapa ili kuisaidia serikali kupitia wizara ya afya kuokoa maisha ya wagongwa wanaohitaji kuongezewa damu katika hosipitali zetu,” alisema Kenan.
Alisema bonanza hilo linalojumuhisha michezo mbalimbali ambapo zawadi ya ng’ombe, mbuzi, medani ,vyeti pamoja na hati za pongezi kwa wale vijana na wananchi waliojitolea ujenzi wa madarasa kwa kutambua mchango wao wa kujitolea nguvu kazi na kuhakikisha wanaleta maendeleo katika jiji la Arusha.
Alifafanua kuwa lengo la bonanza hilo ni kukuza vipaji na michezo pamoja ndani ya Jiji la Arusha pamoja na kuwaleta wana Arusha pamoja hasa katika sekta ya michezo ambapo wanatarajia Arusha iwe sehemu ya kuvumbua vipaji vyote.
Kwa upande wake Afisa Michezo wa halmashauri ya jiji la Arusha,Benson Maneno alisema bonanza hilo limefichua vipaji mbalimbali ikiwepo uongozi wa mpira ambapo hadi sasa Arusha hawana chama cha soka hivyo ni vyema wakawatumia hao kama viongozi.
“Pamoja kuvumbua vipaji kwa bonanza hili kwa kila mchezo fainali zimeingia timu mbilimbili ikiwa maandalizi ya mashindano haya yalianzia katika ngazi ya vitongoji na tarafa hivyo wananchi wajitokeze kushuhudia na kushiriki pamoja ili kuleta mdhikamano,”alisema Afisa michezo huyo.
Hata hivyo bonanza hilo linaendelea katika viwanja vya sheikh Amri Abeid na ni bure huku wajasiriamali wa sekta mbalimbali wakiruhusiwa kwenda kufanya biashara katika fainali za bonanza hilo.