Reading:RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KATIKA MRADI WA UJENZI WA MELI MPYA, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA PAMOJA NA MELI YA MV BUTIAMA KATIKA ENEO LA BANDARI YA MWANZA SOUTH
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA UKAGUZI WA KUSHTUKIZA KATIKA MRADI WA UJENZI WA MELI MPYA, UKARABATI WA MELI YA MV VICTORIA PAMOJA NA MELI YA MV BUTIAMA KATIKA ENEO LA BANDARI YA MWANZA SOUTH
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Tuta la Sehemu inapojengwa Chelezo kubwa yenye uzito wa Tani 4000 kwa ajili ya Ujenzi wa Meli mpya kubwa na ya kisasa itakayohudumu katika Ziwa Victoria kutoka Mwanza kwenda Bukoba, Kisumu(Kenya) na Jinja nchini Uganda.
Meli ya MV Victoria inayotoa huduma katika Ziwa Victoria ikiwa katika ukarabati mkubwa. Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika mwakani mwezi wa tatu na Mashine Engine zake mpya zinatarajiwa kuwasili hivi karibuni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo katika eneo la tuta la ujenzi wa Chelezo ya kujengea Meli hio kubwa na ya kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Meli ya MV Victoria ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa katika eneo la Bandari ya Mwanza South.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wafanyakazi wa Bandari ya Mwanza pamoja na Wabeba mizigo Makuli kuhusu ujenzi wa Meli hizo. PICHA NA IKULU