…………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
SERIKALI kupitia Wizara ya kilimo imefanya kikao cha pamoja na wadau wa kilimo kuhusu mradi wa miaka mine wenye thamani ya Euro Milioni 100 .
Akizungumza na Waandishi wa habari Leo Februari 17,2021 jijini Dodoma mara baada ya kikao hicho Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa lengo la kikao kazi hicho na Wadau wa kilimo ni kuangalia maeneo gani uwekezaji wa fedha unahitajika zaidi .
Bashe amesema kuwa sehemu kubwa ya fedha katika mradi huo wa miaka minne inaenda kwenye miundombinu ya barabara ambapo kiasi cha Euro Milioni 48 zitatumika kitu ambacho ni muhimu sana hasa kwenye chai.
“Tumekuwa tukipoteza kiasi cha kilo mil.4 za chaikwa mwaka ikitupwa kutokana na kuwepo kwa changamoto ya miundo mbinu ya barabara hivyo fedha hizo zitasaidia kuondokana na chanagamoto hii.
Hata hivyo amesema kuwa wanapoenda kumfundisha mkulima inatakiwa kupatikana kwa matokeo hayo mapema zaidi .
“Kila anayeweka fedha kwenye kilimo tunataka kujua anaiweka wapi na matarajio yake ni yapi ili kuweza kuepuka muingiliano ambao unakuwa hauna mantiki”amesema Bashe
“Mradi huu unatarajia kuingiza miche mil 1.5 ya chai ,hivyo uwekezaji huu lazima tuone matokeo yake,nahii itatuondolea tatizo kubwa lililopo kwenye sekta ya chai”amesisitiza
Kwa upande wake mratibu mradi wa MARKUP Safari Fungo amesema wamejikita zaidi katika kusaidia taasisi za kilimo kutafuta masoko na kuvutia mitaji kutoka nje ili kuvutia wawekezaji.
“Mradi huo wa miaka minne unaofadhiliwa na umoja wa Ulaya unaratibiwa na Taasisi ya MARKUP,AGRICOM,Selfier na Solidat.