MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wameanza vyema hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, AS Vita Uwanja wa Marty’s Jijini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Bao la Simba limefungwa na dakika ya 61 na Mshambuliaji wao Chriss Mugalu kwa njia ya Penalti baada ya beki wa AS Vita, Ousmane kuunawa mpira uliopigwa na kiungo Luis Miquissone.