Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma Meja Msitaafu Johnick Salingo akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Dodoma walipotembelea kuona utendaji kazi wa miradi mbalimbali katika kuhudumia wananchi katika jiji la Dodoma.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma Bi Diana Madukwa akizungumza akizungumza katika soko la Ndugai wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya Wilaya ya CCM Dodoma walipotembelea kuona utendaji kazi wa miradi mbalimbali katika kuhudumia wananchi katika jiji la Dodoma.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ambaye ni mchumi wa jiji la Dodoma Charles Ruhembe akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Dodoma walipotembelea kuona utendaji kazi wa miradi mbalimbali iliyopo katika jiji la Dodoma katika kuhudumia wananchi katika jiji la Dodoma.
Meneja wa Kituo kikuu cha Mabasi Dodoma Abedi Msangi akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Dodoma walipotembelea kuona utendaji kazi wa miradi mbalimbali katika kuhudumia wananchi katika jiji la Dodoma.
Katibu wa umoja wa wafanyabiashara katika masoko rasmi Idd Maumba akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Dodoma walipotembelea kuona utendaji kazi wa miradi mbalimbali katika kuhudumia wananchi katika jiji la Dodoma.
………………………………………………………………………………………………….
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Kamati ya siasa ya Wilaya ya Dodoma imemuagiza meneja wa Kituo kikuu cha mabasi cha jijini Dodoma bwana Abedi msangi kuainisha changamoto zote zilizopo katika stendi hiyo zinazopelekea kutofanya kazi kwa ufanisi kwa stendi kama ilivyokusudiwa, ili changamoto hizo zipelekwe katika ngazi husika na kuzitatua.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma Meja Mstaafu Johnick Salingo wakati Makati ya siasa ilipotembelea miradi ya kimkakati pamoja na masoko ya jiji la Dodoma kuona utendaji kazi wake katika kuhudumia wananchi.
Amesema Serikali imetumia fedha nyingi katika miradi hiyo lakini bado kunachangamoto nyingi ambazo zipo katika miradi hiyo na kusababisha kutofanya kazi kama ilivyokusudiwa pindi inapotekelezwa na serikali.
“nataka changamoto zote ziainishwe nataka meneja hapa changamoto zote zinazopelekea stendi hii kutofanya kazi kama ilivyokusudiwa ziainishwe na nizipate ili tukae pamoja na mamlaka husika zitatuliwe haraka” amesema
Aidha wakiwa katika soko kuu la Ndugai kamati imeagiza wasimamizi wa soko kuhakikisha wanaweka sawa miondombinu yote ambayo haijakamilika kuhakikisha inakamilika ili wafanyabiashara ambao hawajahamia katika soko hilo wahamie haraka.
Wasimamizi wa masoko wametakiwa kuyasimamia na kuhakikisha masoko yote yanakuwa safi kuepusha magonjwa yanayoweza kusababishwa na uchafu, sambamba na kuyasimamia ipasavyo masoko hayo yaweze kufanyakazi na kwa utaratibu mzuri.
Pia kamati imezitaka mamlaka husika kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri wa kuwaratibu wafanyabiashara wadogo katika maeneo yao ili wafanye kazi kwa utaratibu na kwa kuzingatia usafi na usalama wao na watu wengine.
“Nataka kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wafanye kazi zao kwa utaratibu mzuri pia vitambulisho vya ujasiliamali vilivyotolewa na Rais viheshimiwe” amesema.
Ameongeza kuwa “Pia mamlaka mfanye kazi kwa kushirikiana katika kutekeleza majukumu yenu sio kila mamlaka inafanya kazi kivyake hii ndio inaleta mikanganyiko katika maeneo mengi” amesema.
Meneja wa kituo kikuu cha mabasi Dodoma Abedi Msangi ameiambia kamati kuwa kituo cha mabasi kinauwezo wa kuhudumia mabasi 100 kwa wakati mmoja na kimekuwa kikihudumia mabasi mia tatu 300 kwa siku kutoka mikoa mbalimbali.
Amesema bado kuna changamoto kwani baadhi ya watoa huduma kushindwa kufuata matakwa yaliyowekwa katika kituo hicho hasa katika utaratibu wa kutolea huduma katika ofisi walizopewa na wafanyabiashara kuhamia eneo hilo kwa wale waliochukua vizimba wasijue kuwa mkataba unaendelea tangu aliposaini mkataba na jiji.
Katika ziara hiyo kamati ya siasa imetembelea kituo kikuu cha mabasi, Soko la Ndugai, soko la saba saba, soko la chang’ombe, Maisha plas, Chadulu B, Shule ya msingi Hombolo na shule ya msingi mkapa.