Meya wa jiji la Arusha Maxmillan Iranq’e akiongea na waandishi wa habari katika maonesho nne ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea mkoani Arusha.
Meya wa jiji la Arusha Maxmillan Iranq’e akiwa katika banda moja wapo lililopo katika mainesho hayo.
Meya wa jiji la Arusha Maxmillan Iranq’e akiwa katika banda la Baraza Ia mifuko ya progaramu za uwezeshaji wananchi kiuchumi
……………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Jiji la Arusha limefanya makubaliano ya kukutana na mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kuweza kujenga jukwaa la pamoja la kuwasaidia wajasiriamali.
Hayo ya yameelezwa na Mstahiki Meya wa jiji hilo Maximilan Iranq’e wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea mabanda katika maonesho ya nne ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea mkoani Arusha.
Alisema kuwa katika jukwaa hilo watahakikisha kwamba watawavuta wajasiriamali wote wadogo waliopo mtaani na kuwapa elimu pamoja na mikopo.
“Serikali ina kila sababu ya kuwasaidia wananchi waweze kuinua uchumi wao ambapo watapa elimu ya jinsi ya kufanya biashara na kuwapa mikopo Ili kuweza kukuza uchumi wao na wa taifa kwa ujumla,” Alisema Meya.
Alisema skuwa serikali inajukumu la kuwalinda wafanyabiashara wake, wajasiriamali na watu wanaoanzisha viwanda ambapo suala la kuzuia bidhaa za nje litaaenda taratibu hadi bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zitakapoweza kukidhi mahitaji.
“Tukisema leo tuzuie kila kitu kinachotoka nje sidhani Kama hawa wazalishaji wa ndani wanaweza kutosheleza soko na huwa serikali haikurupuki bali inafanya utafiti kwanza,” Alieleza.
Aidha alisema kuwa maonesho hayo ni maonesho yanayohitajika sehemu mbalimbali za nchi kwani ni sehemu ambapo watanzania wanapata fursa ya kukutana na taasisi za kifedha pamoja na kujenga mtandao na wafanyabiashara wenzao.
Alisema kuwa wajasiriamali waliopo katika maonesho hayo ni wajasiriamali wazalendo wanaozalisha bidhaa kwa kutumia malighafi za ndani hivyo wanahitaji watanzania wenzao pamoja na serikali kuwaunga mkono.